April 29, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mume wa Marehemu mwimbaji wa Injili ahukumiwa kunyongwa

Osinachi Nwachukwu

 

MAHAKAMA Kuu ya Abuja nchini Nigeria imemhukumu Peter Nwachukwu, mume wa aliyekuwa mwimbaji maarufu wa injili Osinachi, kunyongwa mpaka kufa baada ya kupatikana na hatia ya mauaji. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Hukumu hiyo, iliyotolewa na Jaji Nwosu-iheme, inatolewa miaka mitatu baada ya kifo cha Osinachi kilichotokea mnamo tarehe 8 Aprili 2022. Polisi walimkamata Nwachukwu baada ya mkewe, kufariki akiwa katika hospitali moja jijini Abuja.

Ripoti za awali zilikuwa zimependekeza kwamba mwanamke huyo aliyekuwa na umri wa miaka 42 alikuwa mgonjwa wa saratani ya koo, lakini familia yake ilikataa na kudai kwamba alikuwa mwathirika wa unyanyasaji wa nyumbani na walimshutumu mumewe kwa unyanyasaji na kusababisha kifo cha mke wake.

Peter Nwachukwu

Baadaye mahakama iliamuru kwamba arudishwe kizuizini gerezani. Peter Nwachukwu alishtumiwa kwa “vitendo vya vurugu na kumshambulia mkewe na ufahamu kuwa kifo hicho kitakuwa ni matokeo ya matendo yake.”

Mashahidi 17, pamoja na watoto wawili, waliitwa na upande wa mashtaka wakati wa kesi hiyo. Hati 25 pia zilitolewa kama kithibitisho mbele ya mahakama.

Kesi hiyo imevutia nadhari kwa sababu ya umaarufu wa Osinachi katika muziki wa injili wa Nigeria na jamii ya wakristo.

About The Author

error: Content is protected !!