MTU mmoja, Mkazi wa Kijiji cha Mwanale Wilayani Busega Mkoani Simiyu amekamatwa na anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi Mkoani humo kwa tuhuma za kumtendea mke wake vitendo vya kikatili.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea). Taarifa ya leo 18 Aprili 2026 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani humo imeeleza kuwa chanzo cha kukamatwa mtu huyo aitwaye Magembe Tabu Makulilo ni baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa kupitia mtandao wa kijamii uliokuwa unarusha taarifa kupitia kipindi chenye ujumbe unaosema “SEMA NA WAZIRI”. “Kupitia kipindi hicho, binti mmoja aliomba msaada kwa Waziri wa Sheria na Katiba Dk.Juma Homera kumwokoa mama yake mzazi anayeishi kijiji cha Mwanale ambaye alidai anapigwa kila mara na baba yake mzazi na anahofia anaweza kumuua.” imeeleza taarifa hiyo. Kufuatia hilo, Jeshi la Polisi lilianzisha msako na limefanikiwa kumkamata Magembe ambapo pia, mama aliyekuwa anapigwa amepatikana na taratibu zimefanyika za kumpatia huduma za kiafya sambamba na kupata maelezo yake huku uchunguzi zaidi ukikamilishwa ili hatua zingine ziweze kuchukuliwa dhidi ya mtuhumiwa kwa mujibu wa sheria. Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limeendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa pale wanapoona vitendo vya ukatili vikifanyika kupitia njia mbalimbali zilizowekwa na serikali huku likitoa onyo kwa wale wenye tabia za kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya wake zao kuziacha. Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Fedrick Gama See author's posts Post navigation Equinor yafanya ziara bandari ya Mtwara kutathmini utayari wa mradi wa LNG