KILA kitabu kina zama zake, zama Profesa Ibrahim Lipumba, aliyehuduma kama Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), kwa miaka 32 zimetamatika leo tarehe 22 Februari 2026. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaaam … (endelea).
Profesa. Lipumba si kwa ridhaa yake kupisha uchaguzi mpya bali ni baada ya tangazo la msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi, kueleza kuwa yeye sio mwenyekiti halali kwa kuwa uchaguzi uliomweka kitini ulikuwa batili.
Msimamizi wa uchaguzi huo Said Miraji, amemtangaza Mirambo Yusuf, kuwa ndio Mwenyekiti mpya wa CUF aliyeshinda kwa kupata kura 257 sawa na asilimia 57 za kura zote 448.
Mshindani wa Mirambo Othman Omar Dunga amepata kuwa 177 kama takribani asilimia 40 ya kura zote huku Nkunyunyika Siwale, akiibuka na kura 6, na kura 6 zikiharibika.
Mirambo, ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Kigoma Mjini, amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa nne wa chama hicho, akirithi rasmi mikoba ya Profesa Ibrahim Lipumba katika nafasi hiyo.
Katika uchaguzi huo mshindi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, ni Miraji Mtibwiliko aliyepata kura 264 akimshinda Mohammed Ngulangwa aliyepata kura 88 pamoja na Mussa Mbarouk aliyepata kura 82.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar imechukuliwa na Haroub Mohamed Shamsi aliyepata kura 256, akimshinda Mbarouk Seif Salim aliyepata kura 171, huku Amina Rashid Salim akijitoa kabla ya upigaji kura.
ZINAZOFANANA
Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini yaridhishwa na uzalishaji umeme
Aliyemkamata mhamasishaji vurugu Mbeya atoa ushahidi kesi ya Lissu
Lissu alivyombana shahidi wa 14 wa serikali, neno kwa neno