Spika Mussa Azzan Zungu

 

MBUNGE wa Ilala (CCM), Mussa Azzan Zungu, amechaguliwa rasmi kuwa Spika mpya wa Bunge la Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Zungu amepata kura 378, katika kura 383 zilipigwa. Kura tatu zimeharibika.

Uchaguzi wa Spika wa Bunge la Tanzania umefanyika leo tarehe 11 Novemba 2025, mjini Dodoma.

Kabla ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo, Zungu alikuwa Naibu Spika wa Bunge, chini ya Tulia Akson, ambaye alitangaza kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho, dakika za lala salama.

Katika uchaguzi huo, Zungu alishindana na Jumla ya kura 383 zilipigwa.

Kwa ushindi huo, Zungu anakuwa spika wa nane wa Bunge hilo tangu kuanzishwa kwake, baada ya kuwashinda wagombea wa vyama vingine waliopata jumla ya kura mbili pekee.

Zungu amekuwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 20 sasa. Aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2005.

Mbali na naibu wa spika, Zungu ameshika nyadhifa mbalimbali ikiwamo Mwenyekiti wa Bunge (2012-2021), mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Mambo ya Nje na Usalama na kwamba amefanya kazi na maspika wanne wa Bunge hilo – Samwel Sitta, Anne Makinda, Job Ndugai na Tulia.

Spika huyu mpya ana elimu ya uhandisi wa ndege na amepata mafunzo hayo nchini Tanzania na Canada ambapo anasema, alihitimu mwaka 1982.

Aidha, Zungu ana shahada nyingine za maswala ya diplomasia alizozipata kati ya mwaka 2007 na 2021.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!