March 10, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

ACT Wazalendo Z’bar wataja sababu za kumsusia Mwinyi

Profesa Omar Fakih Hamad, Mwakilishi wa Pandani

 

CHAMA cha ACT-Wazalendo visiwani Zanzibar kimesema Walisusia hafla ya ufunguzi wa Baraza wa Wawakilishi iliyofanyika jana, tarehe 10 Novemba, 2025 kwa kuwa hawakubaliani na matokeo yaliyompa ushindi Rais Dk. Hussein Mwinyi
Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 na 29 Oktoba 2025 na Dk. Mwinyi aliibuka mshindi. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Wajumbe 14 wa Baraza la Wakilishi visiwani Zanzibar kutoka chama hicho cha upinzani, wamesema wangehudhuria hafla hiyo ingekuwa ni sawa na kuwadhihaki Wazanzibari.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake Profesa Omar Fakih Hamad, Mwakilishi wa Pandani, amesema kuwa wameona kuwa kushiriki kwenye hafla hiyo kungewatonesha vidonda wananchi aliodai wamenyang’anywa haki yao ya kuchagua viongozi waliowataka.

“Tulilitafakari tukio la uzinduzi wa Baraza la Wawakilishi na kumpima mtu atakayehutubia baraza (Dk. Mwinyi), majibu yetu yakawa kwa dhuluma na uhuni iliyofanyika katika kilichoitwa uchaguzi wa mwaka huu kuhudhuria tukio lile ni kuwadhihaki kuwachezesha shere kwa kuwatonesha vidonda Wazanzibari walionyang’anywa haki yao,” amesema Profesa Omar.

Profesa Omar amesema kuwa mshindi wa uchaguzi huo amepatikana kwa hila kwa kuwa hata kura zilizopigwa hazikuhesabiwa kwa ujumla wake.

About The Author

error: Content is protected !!