WAKILI Rugemeleza Nshala amesema Mahakama imetoa uamuzi mdogo kuhusu maombi ya Tundu Lissu ya kuomba kuunganishwa katika kesi namba 8323 iliyofunguliwa na Said Issa na wenzake, inayohusu mgawanyo wa mali.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …(endelea).

Akiongea na waandishi wa habari hii leo tarehe 30 April 2026,Wakili Nshala amesema Mahakama imebaini kuwa Lissu aliwasilisha maombi hayo kwa nafsi yake binafsi na si kwa niaba ya nafasi yake ya Uenyekiti wa Chama. Kutokana na hilo, Mahakama imehitimisha kuwa hana maslahi ya moja kwa moja katika shauri hilo, na hivyo kukataa ombi lake la kuunganishwa kwenye kesi hiyo.

Hata hivyo, Mahakama imeeleza kuwa Lissu anaweza kushiriki katika shauri hilo kama shahidi endapo itahitajika.

Katika hatua nyingine, imeelezwa kuwa kesi hiyo sasa ipo mbele ya Jaji Ngunyale, badala ya Jaji Hamidu Mwanga kama ilivyokuwa awali.
Kesi hiyo itatajwa tena 13 Mei 2026 kwa ajili ya maagizo ya Mahakama, ikiwemo kujadili iwapo ilifunguliwa ndani ya muda wa kisheria wa miaka sita tangu mgogoro huo ulipoanza.

Rugemeleza Nshala, amesema Mahakama imetoa uamuzi mdogo kuhusu maombi ya Lissu ya kuomba kuunganishwa katika kesi namba 8323 iliyoletwa na Said Issa na wenzake hao, kuhusu mgawanyo wa mali.

Aidha, kesi hiyo sasa ipo mbele ya Jaji Ngunyale na si Jaji Hamidu Mwanga kama awali ma Itatajwa tena 13 Mei 2026 kwa ajili ya maagizo, ikiwemo kujadili iwapo iliwasilishwa ndani ya muda wa kisheria wa miaka sita tangu mgogoro ulipoanza.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!