Waziri wa Mambo ya nje wa Belarus awasili nchini kwa ziara ya kikazi
WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Belarus Maxim Ryzhenkov, amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia 28 hadi 30 April 2026, kufuatia mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Ryzhenkov amewasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, ambapo alipokewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk Ngwaru Maghembe.

Katika ziara hiyo Ryzhenkov anatarajiwa kufanya mazungumzo ya pande mbili na mwenyeji wake Balozi Mahmoud Thabit Kombo 28 Aprili 2026, jijini Dar es Salaam.
Aidha, atakutana na viongozi wengine wa Serikali kwa lengo la kuendeleza na kupanua ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Belarus pamoja na kukuza ushirikiano wa kiuchumi katika maeneo yenye maslahi ya pamoja.