SERENGETI Premium Apple, bidhaa ya kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL), imekuwa kinywaji cha kwanza tayari kunyweka au Ready-to-Drink (RTD) kilichotengenezwa hapa nchini Tanzania. Kikiwa na asili ya Kitanzania, chapa hii inaleta ladha ya kipekee na hadhi ya juu, iliyobuniwa kuakisi ndoto, mafanikio, na ari ya kusherehekea ya Mtanzania wa kisasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). Ikiwa na mojawapo ya jina la maeneo mashuhuri duniani, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, uzinduzi wa chapa hii unatarajiwa kufanyika katika mandhari halisi na ya kuvutia ya hifadhi hiyo, ukichanganya uzoefu wa kipekee na ladha ya kipekee wa kinywaji hiki. Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo wa kipekee, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Obinna Anyalebechi, alielezea mafanikio hayo kama hatua muhimu kwa kampuni katika kuleta kinywaji cha kwanza cha hadhi ya juu na ladha ya kipekee tayari kunyweka kilichotengenezwa nchini. Alisisitiza kuwa chapa hiyo imeundwa kukidhi mahitaji ya watumiaji wanaotafuta ladha mpya, nyepesi, na yenye kuburudisha, huku pia ikiziba pengo la hadhi na usasa katika soko. “Kwetu SBL, tunabuni bidhaa kuendana na mahitaji ya watumiaji wetu. Tunawasikiliza kwa makini, wanachotaka na namna wanavyotaka kusherehekea nyakati zao muhimu. Hitaji la kuwa na chapa ya nchini, inayojivunia Utanzania na kuakisi hadhi na usasa, ilikuwa dhahiri. Ndiyo maana leo tunazindua Serengeti Premium Apple kukidhi matarajio hayo. “Hiki siyo tu kinywaji, bali ni ishara ya mwelekeo wa Tanzania. Mtumiaji wa leo hanywi tu, anatengeneza kumbukumbu muhimu za maisha. Zaidi ya hayo, uzalishaji wa ndani unachangia kukuza sekta ya viwanda, kuimarisha mnyororo wa thamani, kuzalisha ajira, na kuthibitisha kuwa bidhaa za Tanzania zinaweza kushindana kimataifa,” alisema Anyalebechi Uzinduzi wa Serengeti Premium Apple katika Hifadhi ya Serengeti unadhihirisha fahari ya rasilimali za Tanzania, ukionyesha kuwa hadhi na ubora wa hali ya juu hauhitaji kuagizwa kutoka nchi zingine. Kinywaji hiki kinaweza kufurahiwa katika mazingira ya kifahari kama vile migahawa au bustani nzuri, kikiwa ni cha nyumbani, cha kujivunia, na kilichobuniwa kwa ladha ya kipekee. Kwa kuchagua Hifadhi ya Serengeti kama sehemu ya kufanyia uzinduzi, SBL pia imewekeza kimkakati katika sekta ya utalii, ikiiweka Tanzania kwenye ramani ya kimataifa na kuwahamasisha Watanzania kuendelea kuvumbua hazina ya vivutio walivyonavyo. Kupitia ushiriki wa watengeneza maudhui wakubwa watakaorekodi kila hatua ya tukio, ambapo Serengeti ndiyo mhusika mkuu wa hadithi hii. Picha, video, na simulizi zinabeba ujumbe mmoja mkubwa, kwamba hadhi ya Mtanzania wa kisasa inatoka ndani ya nchi, siyo kuazimwa au kuagizwa, na hii ndiyo fahari halisi ya chapa hii mpya. Akizungumzia uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Ubunifu na Masoko wa SBL, Henry Esiaba, alisema: “Tunajivunia kuzindua bidhaa hii katika Hifadhi ya Serengeti, ambapo tumewaleta pamoja wanawake wenye ushawishi, watengeneza maudhui na wabunifu kutoka sekta mbalimbali, na sauti halisi za utamaduni wetu katika moja ya maeneo ya kuvutia zaidi duniani, huu si uzinduzi wa kawaida, bali ni kusherehekea kile ambacho Tanzania inaweza kutengeneza. Serengeti ndiyo chimbuko la hadithi ya chapa hii. “Kuwapeleka wabunifu hawa wa maudhui kwenye hifadhi ni mwaliko kwetu sote kuendelea kuvumbua ladha na fahari ya Tanzania. Hawatohudhuria tukio pekee, bali pia wataiishi chapa na kupata fursa ya kuwepo eneo ambalo imeanzia. Kwa kufanya hivyo, watakuwa mabalozi wa kwanza kushiriki uzinduzi wa aina yake na kipekee kuwahi kutokea nchini: Sophistication. Bottled.” Akitoa mtazamo wake kama balozi wa chapa, Flaviana Matata alisema: “Kwangu mimi, ni muhimu kushirikiana na chapa inayowakilisha Tanzania ya kisasa, yenye ujasiri, kujiamini, na mtazamo wa kusonga mbele. Ushirikiano huu ni kuhusu kusimulia hadithi na kuunganisha watu. Tunataka kila mtu ajione kuwa ni sehemu ya chapa hii. Na huu ni mwanzo tu, mahali popote pale ambapo watakuwa wakifurahia nyakati nzuri, Serengeti Premium Apple itakuwepo.” Ikiwa na ladha ya tufaa au Apple‘’ iliyo nyororo, yenye kuburudisha na utamu wa kiwango cha juu, Serengeti Premium Apple imetengenezwa maalum kwa nyakati mbalimbali za kufurahia maisha, kuanzia mapumziko ya jioni na marafiki mpaka mitoko ya usiku na burudani tofauti jijini. Ni ladha iliyovumbuliwa mahususi kwa Watanzania wenye ari na ndoto kubwa – ya Kujivunia ya Kitanzania, Yenye Hadhi ya Juu, na Yenye Ujasiri Usiofichika. Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Erasto Masalu See author's posts Post navigation Meridianbet na ustawi wa jamii kupitia msaada kwa wajane