RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko makubwa ya kimkakati katika safu ya washauri wake, akiwateua aliyekuwa Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango na aliyekuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa Washauri wa Rais. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza leo 10 Januari 2026 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwapongeza wanamichezo waliofanya vizuri kimataifa, Rais Samia amefafanua kuwa Dk. Mpango atakuwa mshauri wake katika masuala ya uchumi na miradi, wakati Kassim Majaliwa atakuwa mshauri katika masuala ya kijamii.
Rais amesema amemhamisha Profesa Palamagamba Kabudi kutoka Wizara ya Michezo na kumteua kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum), ili kuratibu na kufanya kazi kwa karibu na washauri hao wapya.
Rais Samia amebainisha kuwa siasa za dunia kwa sasa zinaitazama Tanzania kwa macho mawili- chanya na hasi, hivyo anahitaji safu imara ya washauri wenye uzoefu mkubwa. Ameongeza kuwa Profesa Kabudi atakuwa kiungo muhimu kati ya Rais na washauri hao wawili (Mpango na Majaliwa), akimtaja Profesa kama mtu mtulivu anayeweza “kudeal” na vichwa hivyo vikubwa vya uongozi.
ZINAZOFANANA
RITA yatoa msaada wa vifaa vya ujenzi wa jengo la kituo cha watoto wenye uhitaji Dar
EACOP yazindua mpango wa ‘Msaidie Binti Abaki Shule’ kusaidia hedhi salama
Jumuiya ya Madola sasa kutinga nchini