May 17, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mahakama yaiamuru Serikali kumfikisha Lissu mahakamani

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imekubali ombi la mawakili wa Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) la kusikiliza shauri la uchochezi linalomkabili mahakamani hapo kwa njia ya kufikishwa mahakamani badala ya kusikiliza kwa njia ya mtandao. Anaripoti Faki Sosi Ubwa, Dar es Salaam … (endelea).

Uamuzi huo umetolewa leo tarehe 6 Mei 2025, na Hakimu Mkazi Mkuu Godfrey Mhini. Tarehe 19 Mei 2025, Lissu anatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili usikilizwaji wa mashauri yake.

Uamuzi huo unatokana na mapingamizi yaliyowasilishwa na Jopo la Mawakili wa Utetezi linaloongozwa na Mpale Mpoki. Jopo hilo linapinga shauri hilo kuendeshwa kwa njia ya mtandao.

Mawakili hao wameiomba mahakama hiyo itoe amri kwa Mkuu wa Gereza la Ukonga na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam wafike mahakamani na Lissu apate haki ya kuzungumza na mawakili wake.

Mawakili wa utetezi walipinga mahakamani hapo hoja ya serikali ya kutaka kesi hiyo iahirishe kwa siku 30 ili kutoa nafasi ya upande huo kuzungumza na mteja wao halafu shauri liendelee.

Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili, Job Mrema aliiomba mahakama hiyo iahirishe shauri hilo siku 30 na mahakama iendelee kulisikiliza shauri hilo kwa njia ya mtandao.

Upande huo uliodai mahakama iizingatie hoja ya Jamhuri Shauri liaahirishwe Siku 30 ili kitoa fursa kwa mawakili wa utetezi kuonana na Mteja wao na wajiandae pia katika maelezo ya Awali.

Na hakukuwa na ukiukwaji wa sheria ambayo mahakama imetoa amri yake ya kusikiza Shauri hilo kwa njia ya Mtandao.

Shauri hilo linadhamana na mshtakiwa alipata dhamana hiyo na utaratibu upo sahihi.

Baada ya kusikiliza hoja zote Hakimu Mhini amesema kwa kuwa hoja hizo zitachukua muda mwingi ameahirisha shauri hilo mpaka tarehe hiyo.

Kuhusiana na tafsiri ya kifungu cha 192 cha mwenendo wa makosa ya jinai haikuwa sahihi kwa maana ya shauri liendeshwe kwenye mahakama ya wazi mahakama ipuuze shauri hilo.

Mahakama isitoe amri yoyote ya kumwita Mkuu wa Gereza la Ukonga, Maofisa wa Jeshi la Polisi na maafisa wengine wa magereza wasiitwe kwa sababu hoja hii zinakoukwa sheria na mahakama hii haina mamlaka ya kusikiza hoja zinazohusu jeshi la Polisi na maafisa waliowatuhumu badala yake wangefungua kesi mahakama kuu.

Upande wa Jamhuri umeomba mahakama hiyo kuendelea kusikiliza shauri hilo kwa njia ya mtandao na kwamba sio mara ya kwanza kwa mahakama kufanya hivyo.

About The Author

error: Content is protected !!