
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Medali ya Mother of the Nation Order kutoka kwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).
Medali hiyo iliwasilishwa kwake na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Sheikh Abdullah Bin Zayed Al Nahyan Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 5 Mei 2025.
Aidha, Medali hiyo ni moja kati ya Medali za juu kabisa kutoka kwa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). Medali hiyo hutolewa kutambua mchango Kiongozi katika kuleta maendeleo endelevu kwa jamii yake.
Serikali ya UAE imetambua mchango mkubwa wa Rais Samia katika kuwaletea Watanzania maendeleo endelevu ambayo yanaendana na Sera za UAE za maendeleo endelevu katika kijamii, uwezeshaji wanawake na ushirikiano wa kimataifa.
Sheikh Abdullah aliwasilisha salamu kutoka kwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan na kuwatakia kheri wananchi wa Tanzania katika maendeleo pamoja na ustawi zaidi.
Pia alisisitiza kuimarishwa zaidi uhusiano wa kudumu baina ya nchi hizo mbili na kusisitiza umuhimu wa kupanua ushirikiano katika sekta muhimu.
ZINAZOFANANA
NBC yazindua kampeni ya “NBC Shambani’’ kwa wakulima wa Ufuta Lindi, Mtwara
Msajili Hazina: Ni wakati wa Tanzania kunadi fursa za uwekezaji kimataifa
Polisi waeleza sababu za kumkamata Naibu Katibu Mkuu Chadema