MADAKTARI sita wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure, wamenusurika kifo, kufuatia gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea). Ajali hiyo, imetokea katika Kijiji cha Maremve kata ya Igongwa wilaya ya Kwimba. Madakati waliopata ajali walikuwa wakitoka kutoa huduma kwenye kambi ya madaktari bingwa katika hopsitali ya Icheje wilayani humo. Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi, ni kwamba ajali hiyo imetokea 27 Machi 2026 majira ya saa kumi na mbili na nusu jioni katika barabara ya Jojiro kitongoji na Kijiji cha Maremve, Kata ya Igongwa wilaya ya Kwimba. Walikuwa wakitumia gari lenye namba T.231 AWT, aina ya Toyota Land Cruiser Hardtop iliyokuwa inaendeshwa na Dk. James Nkya. Taarifa ya polisi imeeleza kuwa walipofika katika kijiji hicho walipata ajali wakati dereva alipojaribu kumkwepa mwendesha baiskeli aliyekuwa ameanguka barabarani. “…hapo ndipo gari liliacha njia na kugonga gema la barabara kisha kupinduka na kusababisha majeruhi kwa madaktari hao,” imeeleza taarifa ya polisi. Madaktari waliokuwepo kwenye gari hilo ni pamoja na Dk. James Nkya, Dk.Seif Mmka, Dk. Stanley Makundi, Dk.Avetha Masawe, Dk. Marry Urasa na Dk. Frank Mgeta. Majeruhi wanne bado wanaendelea na matibabu katika hospitali ya Sekou Toure huku wawili wakiruhusiwa. Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza limeendelea kutoa wito kwa makundi yote yanayotumia barabara kuendelea kuzingatia sheria kanuni na taratibu za matumizi sahihi ya barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuzuilika. Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Erasto Masalu See author's posts Post navigation ‘Camp’ ya macho CCBRT Mbagala yavuta mamia ya wakazi wenye matatizo Ibada ya kuuga mwili wa Marehemu Lukuvi mkoani Iringa