Jean-Guy Blaise Mayolas
RAIS wa Shirikisho la Soka, katika Jamhuri ya Kongo (FECOFOOT), Jean-Guy Blaise Mayolas, amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Wallace Karia wa DRC – Kongo, amehukumiwa kifungo hicho, baada ya mahakama kumkuta na hatia, katika makosa kadhaa yakiwamo rushwa, matumizi madarka na utakatishaji wa fedha za maendeleo ya soka.
Hukumu hiyo imeeleza kuwa Mayolas alihusika na vitendo vya utakatishaji fedha na ubadhirifu wa zaidi ya dola 1 milioni (karibu Sh. 2.6 bilioni), zilizotolewa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), kwa ajili ya kuendeleza programu za soka nchini mwake.
Uchunguzi uliofanywa na mamlaka za nchi hiyo, umefichua kuwa Mayola alitumia sehemu ya fedha hizo, kwa matumizi yake binafsi.
Mamilioni hayo ya dola, yalilenga kuendeleza soka la wanawake nchini DRC.
Aidha, mahakama ilimtia hatiani rais huyo wa soka, kwa kughushi nyaraka, kutumia hati bandia na kujihusisha na mgongano wa maslahi.
Mwendesha mashitaka amesema, mpango huo ulihusisha kubadilisha rekodi za fedha na kuelekeza vibaya fedha za maendeleo ya soka la ngazi ya chini.
Katika kesi hiyo, katibu mkuu na mhazini wa FECOFOOT, nao wamehukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani kila mmoja, kwa kuhusika katika ubadhirifu huo.
ZINAZOFANANA
ACT Wazalendo yawasilisha wasiwasi wa hali ya kisiasa UN
MO Dewji aendelea kung’ara orodha ya Mabilionea Afrika
Bashiri mechi zote za Bayern na Meridianbet