Kampuni ya Golden Matrix Group imetangaza rasmi kubadilisha jina lake na kwa sasa itatambulika kama Meridian Holdings Inc, ikiwa ni hatua inayoashiria ukuaji wake kimataifa. Kuanzia tarehe 3 Machi 2026, Meridian Holdings Inc itafanya biashara na Nasdaq Capital Market chini ya alama mpya ya MRDN. Mabadiliko haya yana lengo la kuimarisha taswira ya kampuni mbele ya wawekezaji na wadau wake.
Kubadilika huku kwa jina ni sehemu ya mkakati wa kuoanisha taswira ya kampuni na chapa yake kubwa ya Meridianbet, ambayo imeendelea kuwa uti wa mgongo wa mafanikio ya kundi hilo. Meridian Holdings sasa inasimamia jumla ya taasisi sita zenye nguvu ambazo ni Meridianbet, Expanse Studios, RKings, Classics for a Cause, GMAG na Mexplay. Muundo huu unaonyesha upana wa uwekezaji wake katika michezo ya kubashiri na teknolojia ya michezo.
Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi, Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.
Mageuzi haya yanakuja kufuatia mafanikio makubwa ya upanuzi katika soko la Malta. Kupitia ununuzi wa Fairbet Ltd., Meridianbet imeongeza idadi ya maduka ya rejareja na kufikisha jumla ya vituo 20. Mtandao huo sasa una zaidi ya mashine 60 za kubashiri michezo na mashine 120 za sloti. Hatua hii imeimarisha nafasi yake kama mwendeshaji na mwajiri mkubwa katika soko.
Vilevile, Meridian Holdings Inc. imetangaza mpango wa kuunganisha hisa ili kuboresha muundo wake na kuongeza mvuto kwa wawekezaji wa taasisi. Mkakati huu unalenga kuoanisha thamani ya hisa na viwango vya kimataifa vya sekta ya michezo ya kubahatisha.
Afisa Mtendaji Mkuu, Zoran Milosevic, amesema kuwa mabadiliko ya kuwa Meridian Holdings yanaakisi hali halisi ya biashara ya kampuni leo. Amesisitiza kuwa kwa Meridianbet kuwa chapa kinara na kwa kuzingatia mafanikio ya upanuzi nchini Malta, kampuni imeamua kuunganisha utambulisho wake ili kuwahudumia vyema zaidi wanahisa wake na masoko yote inayofanyia kazi.
ZINAZOFANANA
Fainali ya ushindi kwa mabingwa wa Kasino inapatikana kwa Gates of Love
SBL yazindua rasmi Serengeti Premium Apple, kinywaji cha Kitanzania
Vaso Psycho kukupa nafasi ya mbinu zako kukutana na bahati