Tundu Lissu akiwa mahakamani
TUNDU Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameibua pingamizi la kupinga kutumika kwa sheria ya kuficha mashahidi kwenye shauri la uhaini linalomkabili katika Mahakama Kuu, masjala ndogo ya Dar es Saalam. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Leo tarehe 12 Novemba 2025, kabla ya shahidi wa nne wa serikali ambaye alitambulishwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga, kuwa ni shahidi wa siri aliyepewa jina la P11, Lissu aliwasiisha pingamizia lake alilolijengea msingi wa sheria wa kwamba sheria kama haijachapishwa kwenye gazeti la serikali haipaswi kutumika.
Shauri hilo linalosikilizwa na jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Iringa, Dunstan Ndunguru, akishirikiana na majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde
Lissu ameutaja msingi wa kanuni za kuficha mashahidi umetokana na sheria Na. 194 ya mwenendo wa makossa ya jinai (CPA),
“Kifungu hiki kililetwa na sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali Na. 07 ya 2018. Hii sheria inayoruhusu kuficha mashahidi haijawahi kuchapishwa kwenye gazeti la serikali”
Lissu ameeleza mahakamani hapo “Kifungu cha 14 cha Sheria ya Tafsiri yaSheria kinasema ili sheria ianze kutumika lazima iwe published kwenye gazeti.
“Sheria yenyewe haisemi itaanza kutumika tarehe ngapi hivyo ilipaswa kuanza kutumika siku ilipotangazwa kwenye gazeti la serikali hadi muda huu niliposimama hapa sheria hii haijawahi kutangazwa kwenye gazeti la serikali,”
Awali Lissu alianza na hoja ya majaji kutomuona shahidi na kueleza kuwa namna yoyote ile sheria hairuhusu jambo hilo.
Lissu alidai mahakamani hapo kuwa pamoja kuwa shahidi huyo wa kificho lakini kanuni zinataka shahidi huyo aonwe na mahakimu au majaji wanaosikilizwa.
“Sasa nina pingamizi, waheshimiwa majaji huyo shahidi wa siri anatakiwa asimame kwenye kizimba na sio huko ambako haonekani.
“Napenda kuwafahamisha kwamba hili suala la ulinzi wa mashahidi, nimelitafakari kwa zaidi ya miezi 6 sasa na nimeliangalia kwa makini sana,”amedai Lissu.
Lissu amedai mahakamani hapo kuwa, hakuna shahidi yoyote kwa amri iliyotolewa na mahakama hakuna shahidi hata mmoja ambaye anatakiwa kutoa ushahidi akiwa kwenye kificho badala yake anatakiwa akae kizimbani.
“Naomba nianze na sheria sasa kwamba inasema nini kuhusu hawa wanaoitwa Mashahidi wa siri”
“Kanuni za ulinzi wa mashahidi za Mwaka 2025, zimeeleza hicho kiboksi hapo ni kitu gani kisheria”
Lissu amedai kuwa kanuni ya tatu ya sheria ya kulinda mashahidi inataka kuwepo kwa kizimba maalum ambacho anatakiwa aonwe na hakimu au jaji.
“Nasisitiza isipokuwa kwa Jaji au Hakimu. Sasa swali Je hapo alipokaa shahidi waheshimiwa majaji mnaweza kumuona huyo shahidi?”alihoji Lissu.
“Waheshimiwa majaji kwa macho yangu shahidi hapo haonekani kwa majaji, wala mimi simuoni. Watu pekee wanamjua ni hawa mawakili wa serikali waliomleta akina Katuga” aliongoza Lissu.
Lissu amehoji “kwa misingi gani ya haki katika dunia hii?
Baada ya kuwasilisha pingamizi hilo wakili wa serikali Katuga ameomba mahakama iupe muda upande huo kwa ajii ya kujibu hoja zilizowasilishwa na Lissu. Majaji waliamua kuahirisha shauri na kwa kuwa kikao cha usikilizwaji wa awamu hiyo uliishia leo basi mahakama itapanga tarehe ya kikao kingene.
ZINAZOFANANA
Lissu apinga shahidi wa siri kutoonekana na majaji
Waziri Mkuu, Naibu Spika kuthibitishwa kesho bungeni
Hatujatolewa kwa sababu ya maridhiano -Heche