RAIS wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi amesema kuwa chama hicho hakipo kwa ajili ya kulambishwa asali na wala hakifanyi siasa bali kipo kwa ajili ya kusaidia jamii katika kutafuta haki bila upendeleo wa aina yoyote. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Mwabukusi ametoa kauli hiyo alipokuwa akitoa taarifa yake mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hasani wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya Sheria yenye kauli mbiu isemayo “Tanzania ya 2050 Nasafi ya taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo makuu ya dira ya Taifa ya Maendeleo”katika viwanja vya chinangali Jijini Dodoma.
Rais Mwabukusi amesema kuwa chama hicho kipo kwa ajili ya kuonya,kukemea,kushauri na kupongeza kama itabidi kwa ajili ya manufaa makubwa ya nchi na siyo chama siasa na chama hicho hakifanyi biashara bali kuitetea jamii.
Amesema kuwa TLS ni chama ambacho kinasimamia sheria na hakipo kwa ajili ya kufanya utabiri wala kufurahisha watu wa upande mmoja na kukandamiza upande mwingine bali sheria inasimawa kwa watu wote.
Katika hatua nyingine Mwabukusi amesema kuwa pamoja na serikali kuboresha miundombinu ya kimahakama lakini bado kuna haja kubwa ya kuboresha masirahi ya watumishi wa mahakama hususani mawakili na majaji kwani hao wanawahudumia wananchibkwa ukaribu zaidi.
“Ni ngumu kumuhudumia mwananchi hukiwa na msongo wa mawazo na anayetafuta haki ni mwananchi ambaye wakati mwingine anaweza kuwa hivyo ni bora kuboresha masilahi ya mawakili na mahakimu,” ameeleza Mwabukusi.
Katika hatua nyingine Mwabukusi ameitaka serikali kuona uwezekano wa kuifanya Taasisi ya haki za binadamu na utawala bora kuwa na meno kuwa na meno ili kuweza kufuatilia masuala ya watu wanaopotea,kutekwa,kurejeshwa na watu kuuliwa na wakati mwingine hata pale ambapo panaonekana kutofikiwa kwa kufanya uchunguzi panafikika.
Akizungumzia juu ya vitendea kazi amesema kuwa TLS bado haina vitendea kazi vya kutosha na kwa maana hiyo inafungua milango na madirisha kwa mtu yoyote anayetaka kuwasaidia awasaidie lakini wakitambua kuwa hiyo siyo sehemu ya rushwa bali ni kwa ajili ya kurahisisha ufanyaji wa utetezi kwa Umma na jamii kwa ujumla wake.
Hata hivyo amesema kuwa anaishukuru Wizara ya Katiba na sheria kwa kuwapatia gari na kueleza kuwa gari hiyo itatumiwa kwa ajili ya kufanya kazi ya kutafuta haki kwa watu ambao wanahitaji msaada wa kitaifa.
ZINAZOFANANA
CCM Malinyi yaadhimisha miaka 48, yatoa wito wa maendeleo na nidhamu ya kisiasa
Watendaji daftari la wapiga kura Tanga, Pwani watakiwa kufanya kazi kwa weledi
Wataalam 2,980 wajengewa uwezo kutoa huduma ya afya ya akili