Ana komu wa Chadema afariki dunia
ALIYEKUWA Mjumbe wa bodi ya wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Anna Komu amefariki dunia saa tatu usiku wa jana Jumanne 28 Aprili 2026 jijini Dar es Salaam.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), Amani Golugwa ameithibitishia kifo cha mwanachama wake, aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu na mgombea mwenza wa urais 2005.
Maulida alikuwa ni mmoja ya waliofungua kesi dhidi ya bodi ya wadhamini ya Chadema, wakidai chama hicho kimekuwa kikiitenga Zanzibar katika kuendesha shughuli zake ikiwemo suala la rasilimali fedha.
Kesi hiyo inaendelea Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, Anna Komu aliteuliwa na Chadema kuwa mgombea mwenza wa urais baada ya Jumbe Rajab Jumbe kufariki dunia zikiwa zimesalia nne kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu 26 Oktoba 2005.