Ripoti ya tume ya Jaji Chande haijasomwa hadharani-Madeleka
Wakili na mwanaharakati Peter Madeleka amesema kuwa hadi sasa ripoti kamili ya tume iya Jaji Chache liyoundwa kuchunguza matukio yaliyotokea Oktoba 29 nchini chini ya Rais Samia Suluhu Hassan haijawahi kusomwa hadharani, tofauti na inavyoaminika na baadhi ya wananchi.Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam ….(endelea).
Madeleka ameeleza kuwa kile kilichowasilishwa mbele ya umma si ripoti yenyewe, bali ni hotuba ya mwenyekiti wa tume ya matukio ya Oktoba 29,wakati wa kukabidhi ripoti hiyo kwa Rais.
Amesisitiza kuwa hatua hiyo imeacha maswali mengi kwa umma, ambao ulikuwa ukitarajia kupata maelezo ya kina kuhusu uchunguzi huo.
“Ripoti haijawahi kusomwa popote. Ile iliyosomwa ni hotuba ya mwenyekiti wakati wa kukabidhi ripoti,” ameeleza Madeleka.
Aidha, ameeleza wasiwasi wake juu ya uwezekano wa ripoti hiyo kutosomwa kabisa hadharani, akirejea kauli ya Rais kwamba ripoti hiyo ni mali yake.
Kwa mujibu wa Madeleka, kauli hiyo inaweza kuashiria kuwa uamuzi wa kuiweka wazi au kutoiweka uko mikononi mwa mamlaka ya juu ya nchi.