MCHEZO wa pili wa Dabi ya Kariakoo kwenye Ligi kuu bara kwa msimu wa 2025/26 kati ya wenyeji Simba SC dhidi ya mahasimu wao, Young Africans SC utapigwa Mei 03, 2026 saa 12:00 jioni katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo ambao ndio uwanja wa nyumbani wa Wekundu hao wa Msimbazi.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Taarifa ya leo 24 Aprili 2026 iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeeleza kuwa mchezo huo ambao awali ulipangwa uchezwe katika dimba la Benjamin Mkapa 3 Mei 2026 umehamishiwa Meja Jenerali Isamuhyo kwa sababu uwanja wa Benjamin Mkapa upo kwenye matengenezo.
TPLB imesema Simba SC na na Yanga SC pamoja na wadau wengine wa Ligi Kuu ya NBC wamepatiwa taarifa zote kuhusiana na mabadiliko ya uwanja wa mchezo huo na maandalizi yake yanaanza mara moja ili kuhakikisha unafanyika katika kiwango cha juu kinachoendana na hadhi ya michezo mikubwa ya Ligi ya sita kwa ubora barani Afrika.
ZINAZOFANANA
Latra yaonya wanaopandisha nauli kabla ya mei mosi
Searching for the ‘angel’ who held me on Westminster Bridge
The full story of Thailand’s extraordinary cave rescue