MFALME wa Morocco Mohammed wa Sita amewasamehe zaidi ya wakulima 4,800 wanaoshtumiwa kulima bangi kinyume cha sheria. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa… (endelea).
Wizara ya sheria ya taifa hilo imesema jana Jumatatu Mfalme huyo ametoa msamaha kwa watu 4,831 waliopatikana na hatia, kushtakiwa au kutafutwa katika kesi zinazohusiana na kilimo cha bangi.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, Morocco ambayo ni mzalishaji mkubwa zaidi wa bangi duniani, ilipitisha sheria mwaka 2021 kuhusu uzalishaji wa bangi na kuitumia kama matibabu, na kuruhusu kilimo cha bangi katika mikoa ya vijijini katika eneo la kaskazini mashariki la Rif.
Wakati hali ikiwa hivyo, na lengo la kupiga vita biashara haramu, nchi hiyo inataka kujiweka kwenye soko la kimataifa la bangi halali ambayo imekuwa ikizalishwa katika eneo la Rif kwa karne kadhaa na kuzisaidia familia kati ya 80,000 na 120,000.
Msamaha huo unalenga kuwaruhusu wahusika kujumuika katika mkakati huo mpya.
Morocco ilianzisha idara maalum, ANRAC, ili kuunda kilimo halali na usafirishaji wa bangi kwa madhumuni ya matibabu, dawa na viwanda.
Idara hiyo tayari imetoa vibali zaidi ya 200 vya kusindika bangi, kuagiza mbegu kutoka nje na kuuza bidhaa hiyo nje ya nchi.
ZINAZOFANANA
Putin, Pezeshkian waahidi kuimarisha uhusiano
Gachagua kunyoa au kusuka Bunge la Seneti wiki ijayo
Watu 78 wafariki baada ya boti kuzama Kongo, 58 waokolewa