
IDADI ya watu waliofariki katika ajali iliyotokea tarehe 28 Juni, 2025 katika eneo la Sabasaba, Same mjini ikihusisha basi la Kampuni ya Chanel One lililokuwa likitokea Moshi kwenda Tanga na basi dogo aina ya coaster imefikia 39. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Magari hayo yaligongana uso kwa uso na kuwaka moto na kuteketeza baadhi ya abiria waliokuwamo kwenye magari hayo yaliyopata ajali wilayani Same, mkoani Kilimanjaro
Akizungumza leo tarehe 30 Juni 2025, mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema, vifo vimeongezeka kutoka 38 vya awali na 39 baada ya majeruhi aliyekuwa akiendelea na matibabu kufariki dunia.
Akizungumzia hali za majeruhi, amesema mpaka sasa watu 22 kati ya 28 wameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya afya zao kuimarika.
Amesema vipimo vya vinasaba (DNA) vya miili 33 vimeshapelekwa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa utambuzi na kuikabidhi kwa familia kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Mabaki ya miili iliyotambuliwa mpaka sasa ni mitano huku mingine 33 ikifanyika vipimo hivyo kutokana na kuharibika.
ZINAZOFANANA
Rostam: Sekta binafsi iko tayari kuisadia ukuaji wa uchumi wa dola trilioni moja
Mohamed Abdulrahman: Gwiji la utangazaji DW laanguka
Kwaheri Joshua Nassari, Karibu DC Lawuo