CHAMA kikuu cha upinzani nchini Malawi cha Democratic Progress jana Jumapili kimemuidhinisha Rais wa zamani taifa hilo, Peter Mutharika kuwa mgombea wake katika uchaguzi wa urais mwaka ujao. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Mutharika mwenye umri wa miaka 84, ambaye alikuwa rais wa nchi hiyo kuanzia mwaka 2014 hadi 2020, alisema katika hotuba yake ya kukubali uteuzi, kwamba yeye na chama chake watarekebisha uchumi ambao ukuaji wake si mzuri na umekumbwa na uhaba wa fedha za kigeni ambao umesababisha ukosefu wa mafuta na dawa.
Mutharika atakabiliana na Rais Lazarus Chakwera wa chama cha Malawi Congress, ambaye atakuwa akiwania muhula wa pili katika uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 16 Septemba 2025.
“Tunatokea katika historia ya ushindi kutoka upinzani. Tutafanya hivyo-hivyo mwaka ujao. Tunakuja kurekebisha uchumi,” Mutharika aliuambia mkutano mkuu wa kitaifa wa chama chake katika mji mkuu wa kibiashara Blantyre.
ZINAZOFANANA
Putin, Pezeshkian waahidi kuimarisha uhusiano
Gachagua kunyoa au kusuka Bunge la Seneti wiki ijayo
Watu 78 wafariki baada ya boti kuzama Kongo, 58 waokolewa