RAIS Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali ikiwemo mawaziri wanne. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatano na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dk. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa na kuhamishwa vituo vya kazi ni pamoja na Prof. Palamagamba Kabudi ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria na William Lukuvi ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu). Wawili hao walitupwa nje ya Baraza la mawaziri tangu tarehe 8 Januari 2022 huku Rais Samia akiutangazia umma kuwa amewapa kazi maalumu. Prof. Paramagamba Kabudi Katika taarifa ya leo pia Jenista Mhagama ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya na kuchukua nafasi ya Ummy Mwalimu ambaye hajapangiwa kazi nyingine. Kabla ya uteuzi huu, Mhagama alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) na Balozi Dk. Pindi Hazara Chana ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utali. Kabla ya uteuzi huu, Chana alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria, anachukua nafasi ya Angellah Kairuki ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais. Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Erasto Masalu See author's posts Post navigation Mbowe: Viongozi wote Chadema hawataripoti polisi Samia afagia ofisi ya AG, Hamza amrithi Feleshi