MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema viongozi wote wa chama hicho hawatokwenda kuripoti polisi kama ambavyo wameelekezwa baada ya kujidhamini wenyewe na wengine kudhaminiwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mbowe ametoa msimamo huo leo Jumatano wakati akizungunza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu tukio la viongozi wakuu na wafuasi zaidi ya 520 waliokamatwa mapema wiki hii kwa tuhuma za kukaidi agizo la kutofanya kongamano la maadhimisho ya siku ya vijana duniani.
“Polisi wanatutaka tuende turipoti vituo vyao nyakati tofauti, tunatumia falsafa ya Thomas hobbes kuhusu civil disobedience kwamba hatutaki kuwa makondoo. Nawaambia viongozi wetu wote hatutarudi polisi kwenda kuripoti polisi,” amesema.
Amesema hatokwenda polisi kufuata mashtaka ya uongo, kughushi na kudhalilisha.
Katika tukio hilo, Mbowe na Mwenyekiti wa Bavicha, John Pambalu walitakiwa kuripoti kituo kikuu cha polisi Dar es Salaam tarehe 19 Agosti mwaka huu.
Lissu alitakiwa kuripoti tarehe 16 Agosti, wakati Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika alitakiwa kwenda kuripoti tarehe 15 Agosti mwaka huu.
ZINAZOFANANA
Malasusa: Utekaji, mauaji yafike mwisho
BAKWATA yataka serikali kuchunguza mauaji na utekaji
Mpina amvaa Bashe kivingine