BENKI ya CRDB kupitia kitengo chake cha kadi, imetangaza washindi 7 waliopata fursa ya kusafiri kwenda kushuhudia fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Marekani.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea). Akizungumza wakati wa kutangaza washindi hao, Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Kadi wa benki hiyo Karington Chahe, alisema kuwa washindi wamepatikana kupitia kampeni maalum iliyolenga kuhamasisha matumizi ya kadi za benki hiyo katika miamala ya kila siku ambapo washindi 3 wamejishindia tv inch 85 na dekoda yake na washindi 4 wamepata fursa ya kusafiri kushuhudia fainali hizo za kombe la dunia 2026. Alieleza kuwa kampeni hiyo imelenga kuwapa wateja thamani zaidi kwa kuwawezesha kushinda zawadi mbalimbali, ikiwemo safari ya kimataifa ya kwenda kushuhudia michuano hiyo mikubwa ya soka duniani. Chahe amewataka Watanzania kuendelea kutumia huduma za kidigitali, hususan Tembo Card, ili kurahisisha miamala yao na kujiongezea nafasi ya kushinda zawadi nyingine zitakazotolewa na benki hiyo siku zijazo. Aliongeza kuwa CRDB itaendelea kubuni na kuendesha kampeni kama hizo kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha za kisasa pamoja na kuwazawadia wateja wake waaminifu. Kwa upande wao, baadhi ya washindi walieleza kufurahishwa na ushindi huo na kuishukuru benki hiyo kwa kuwapatia fursa ya kipekee ya kushuhudia fainali za Kombe la Dunia moja kwa moja nchini Marekani. Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Fedrick Gama See author's posts Post navigation Casino ilivyokuwa sehemu ya burudani ya kidijitali nchini