
RAIS Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali ikiwemo mawaziri wanne. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatano na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dk. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa na kuhamishwa vituo vya kazi ni pamoja na Prof. Palamagamba Kabudi ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria na William Lukuvi ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).
Wawili hao walitupwa nje ya Baraza la mawaziri tangu tarehe 8 Januari 2022 huku Rais Samia akiutangazia umma kuwa amewapa kazi maalumu.

Katika taarifa ya leo pia Jenista Mhagama ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya na kuchukua nafasi ya Ummy Mwalimu ambaye hajapangiwa kazi nyingine.
Kabla ya uteuzi huu, Mhagama alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) na Balozi Dk. Pindi Hazara Chana ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na
Utali. Kabla ya uteuzi huu, Chana alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria, anachukua
nafasi ya Angellah Kairuki ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais.
ZINAZOFANANA
Kadinali Robert Prevost atangazwa kuwa Papa mpya
Bunge la Ulaya laitaka Tanzania kumuachia huru Lissu
Chatanda ashuhudia utiaji saini wa Bil 13.3 kuboresha miundombinu Rufiji