March 14, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Ronaldo akimbia vita Saudia, aelekea Madrid

Ndege ya Cristiano Ronlado

 

NDEGE binafsi ya mchezaji nyota wa soka wa kimataifa, Cristiano Ronaldo, imeondoka ghafla nchini Saudia Arabia. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa zinasema, ndege ya Ronaldo, imeondoka Riyadhi usiku wa kuamkia leo, kuelekea Madrid, nchini. Hispania.

Kuondoka kwa ndege hiyo kutoka Riyadh kuelekea Madrid, kumefungua mjadala mpana kuhusu hali ya usalama nchini Saudi Arabia, wakati huu ambako mvutano wa kijeshi ukiendelea kuongezeka eneo la Mashariki ya Kati.

Mvutano huo, unatokana na hatua ya Marekani na mshirika wake mkuu Israel, kuishambulia kijeshi Iran, ambayo nayo inalipiza kisasi kwa kushambulia maslahi ya Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati.

Taarifa zinasema, Riyadh imekumbwa na mashambulizi ya anga yanayohusishwa na mvutano huo kati ya Marekani na Iran.

Pamoja na kutokuwapo tamko rasmi linalothibitisha kuwa Ronaldo ameondoka nchini humo kwa sababu za kiusalama, lakini kuondoka kwa ndege yake, kunaonyesha mwanasoka huyo hayuko tena Riyadhi.

Ronaldo anaishi Riyadh na familia yake tangu alipojiunga na klabu ya Al-Nassr FC, na kwamba amekuwa sura muhimu ya kampeni ya Saudi Arabia kujitangaza kama kitovu kipya cha michezo ulimwenguni.

Kuondoka kwa mwanamichezo huyo, hata kwa muda, kunaweza kutafsiriwa kama ishara ya tahadhari katika kipindi hiki cha sintofahamu ya kijeshi.

Kwa mujibu wa data za ufuatiliaji wa safari za anga, ndege aina ya Bombardier Global – Express 6500, iliondoka Riyadh majira ya saa 8:00 usiku, ikapitia anga ya Misri na Bahari ya Mediterania kabla ya kutua Madrid saa 1:00 asubuhi.

About The Author

error: Content is protected !!