Amir Mhando, Mwenyekiti wa TASWA

 

MAGWIJI wa habari za michezo nchini wanatarajia kukutana Aprili 24, 2026 jijini Dar es Salaam kwenye warsha ya kujadili mustakabali wa uandishi wa habari za michezo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Warsha hiyo ya siku moja imeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA ikiwa na mada kuu isemayo: “The Future of Sports Journalism (Mustakabali wa Uandishi wa Habari za Michezo)”, inatarajiwa kuhusisha washiriki 60 na itaanza saa 3 asubuhi Ukumbi wa Jiji Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Katika kuhakikisha warsha hiyo inaleta tija na maarifa mapana kwa washiriki, TASWA imealika wataalamu mbalimbali kutoa mada tofauti ndani ya wigo wa mada kuu ya warsha na kisha kutakuwa na mjadala.

Miongoni mwa walioalikwa kutoa mada wapo magwiji wa habari nchini, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wataalamu wa habari za kidijitali

Washiriki ni waandishi na watangazaji wabobevu wa habari za michezo, wahariri, waandishi waandamizi na waandishi wa habari chipukizi wakiwemo wale wa mitandao ya kijamii wanaotambuliwa na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB).

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!