MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini Tanzania (Latra) imetoa onyo kwa watoa huduma wanaotoza nauli mpya kabla ya muda rasmi, ikisema hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea). Onyo hilo linakuja baada ya kuibuka kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi, hasa wa jiji la Dar es Salaam, kwamba baadhi ya vyombo vya usafiri, hususan daladala, bajaji na bodaboda, zimepandisha nauli kwa kigezo cha tangazo la Serikali. Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Latra, Salum Pazzy amesisitiza kuwa utekelezaji rasmi wa nauli mpya utaanza Mei Mosi kama sheria inavyoelekeza. “Kwa mujibu wa sheria, nauli mpya huanza kutumika baada ya siku 14 tangu tangazo rasmi la Serikali, hivyo muda huo bado haujakamilika na utekelezaji unaanza Mei Mosi,” amesema Pazzy. Pazzy amesema watoa huduma wa usafirishaji wanaotoza nauli mpya kabla ya tarehe hiyo wanakiuka sheria na wanaweza kuchukuliwa hatua Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Fedrick Gama See author's posts Post navigation Zawadi kubwa ya Samsung A26 inakusubiri Meridianbet