TUME ya Uchunguzi ya matukio ya Oktoba 29 inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake rasmi kwa Rais Samia Suluhu Hassan 23 Aprili 2026.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea). Taarifa hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Othman Chande, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Tume. Jaji Chande amesema kuwa ripoti hiyo imekamilika na itawasilishwa kama ilivyopangwa, huku akisisitiza kuwa nyaraka hiyo itakuwa na uzito mkubwa katika kutoa mwelekeo na hatua zinazopaswa kuchukuliwa kufuatia matukio ya Oktoba 29. Kwa mujibu wa Jaji Chande, kazi ya Tume hiyo imehusisha ukusanyaji wa ushahidi, maoni ya wadau mbalimbali pamoja na uchambuzi wa kina wa taarifa zilizokusanywa, ili kuhakikisha kuwa ripoti inayowasilishwa inakuwa ya kuaminika na yenye manufaa kwa Taifa. Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Fedrick Gama See author's posts Post navigation Chadema yamshtaki Samia kwa wanawake viongozi wa Afrika Taifa litamkumbuka Askofu Mfumbusa kwa kuunganisha dini na Madhehebu mengine-Nchimbi