RAIS wa Marekani, Donald Trump, amechapisha video ya dakika nane kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social na kuthibitisha kuwa taifa lake, limehusika katika shambulizi dhidi ya Iran. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Katika taarifa yake asubuhi ya leo, Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz ametangaza “hali maalum na ya dharura” kote nchini Israel.
Milipuko mitatu imesikika katikati mwa jiji la Tehran, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran.
Shirika la habari la Fars linasema, limepokea taarifa kwamba makombora kadhaa yamepiga eneo mji mkuu wa Iran.
Taarifa zaidi za milipuko mjini Tehran sasa zinaibuka katika vyombo vya habari vya Iran.
Shirika la habari la Fars linaloshirikiana na serikali nchini Iran linaripoti kuwa milipuko mingine ilisikika kaskazini na mashariki mwa Tehran.
Israel imefunga anga yake kwa safari za ndege za kiraia kufuatia shambulio dhidi ya Iran, kulingana na ripoti katika vyombo vya habari vya Israeli.
Nalo shirika la habari la Tasnim, ambalo lina uhusiano na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, linaripoti anga ya Iran pia imefungwa.
Majid Akhavan, msemaji wa Shirika la Usafiri wa Anga nchini Iran, alitangaza: “Kulingana na Notam iliyotolewa, anga ya nchi nzima imefungwa hadi ilani nyingine.”
Jeshi la Israel lilitangaza kuwa limewasha ving’ora vya tahadhari ya mashambulizi ya anga katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Jeshi limesema, “kuwaandaa wananchi kwa uwezekano wa kurushwa kwa makombora kuelekea Israel” kama hatua ya kulipiza kisasi.
ZINAZOFANANA
Kardinali Pengo aagwa kanisani kwake
‘Meli iliyokamatwa na Cocaine nchini El Salvador ilisajiliwa nchini’
Wamekimbilia Mahakama ya Rufani ili kumkomoa Lissu, haikubaliki kisheria