CHAMA cha Wasambazaji wa Bidhaa na Watoa Huduma Migodini (TAMISA) kimezitaka kampuni za kigeni zinazowekeza katika sekta ya madini nchini kuhakikisha zinatoa kipaumbele kwa Watanzania katika ajira, utoaji wa huduma na usambazaji wa bidhaa, kwa mujibu wa sheria ya maudhui ya ndani (Local Content). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa TAMISA, Peter Kumalilwa, alisema kuwa lengo la uwekezaji katika sekta ya madini ni kuhakikisha Watanzania wananufaika moja kwa moja na rasilimali zao kupitia ajira, zabuni na fursa za kiuchumi zinazotokana na shughuli za migodini.
Alisema kuwa bado kuna changamoto katika utekelezaji wa sera ya maudhui ya ndani, huku akibainisha kuwa TAMISA inaendelea kupokea taarifa kuhusu baadhi ya migodi inayokiuka miongozo hiyo kwa kutoa zabuni kwa kampuni zisizo na umiliki wa wazawa, pamoja na kuweka masharti magumu yasiyo rafiki katika mifumo ya manunuzi.
“
ZINAZOFANANA
Tuzo za ZICA: NBC yaibuka kinara uwezeshaji miradi ya ujenzi Zanzibar
Rais Museven kuwasili Tanzania kesho kwa ziara ya kikazi
Spika aitaka Serikali iweke maeneo ya kihistoria ya Papa Leo XIV