February 3, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Kushtakiwa kwa Mwandambo, kusafirishwa mpaka Dar kwaibua mashaka

Clemence Mwandambo

 

NI siku 12 tangu Mwanaharakati maarufu mtandaoni mwalimu wa shule ya Chekechea, Clemence Mwandambo, ambapo tarehe 10 Januari 2026, ameachiwa kwa dhamana huku akiwa chini ya uangalizi wa kutofanya kosa lolote. Kumewatia mashaka familia yake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI TV, Philip Mwakilima, wakili wa Mwandambo, amesema baada ya kusambaa kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu maombi hayo ndio maana wamemuachia kuficha aibu kabla Mahakama haijawaamuru.

Amesema kuwa kitendo cha Jeshi la Polisi kumsafirisha kutoka Mbeya mpaka Dar es Salaam, bila kuipa taarifa familia yake au mawakili wake kinaziidi kutia mashaka.

“Taarifa ambazo nimezipata kwa mdogo wake ambaye yupo Kahama kwamba wamepigiwa simu asubuhi wakamwakee dhamana , hata ndugu hawajui kama Mwandambo amepelekwa jijini Dar es salaam, ndio maana ilikuwa tukitaka kumuona walikuwa hawataki kumbe walikuwa hawataki kwa sababu alikuwa hayupo Mbeya,” amesema Mwakilima.

Ameongeza “Nini kimewafanya wasitoe taarifa kwa ndugu zake kama yupo Dar es salaam haya mambo yanaleta sintofahamu katika sura ya nchi … haya mambo yanaendelea kuondoa imani kwa jeshi la polisi umma unatazama umma unaona”

“Sisi habari kama yupo kwenye kituo cha Polisi cha Chang’ombe nimezijua leo asubuhi ndio nikamwambia wakili mwenzangu afuatilie polisi mara baada ya kuona tumepeleka maombi ya kumtaka IGP na wenzake wampe dhamana au wamempeleke mahakamani ndio maana wakaamua kumuacha ili kuificha aibu”

Amesema kuwa anashangazwa na kitendo cha Mwandambo kutolewa mahakamani kisha kurejeshwa kwenye mahabusu ya polisi, “ikiwa suala la dhamana halijakamilika kwanini hawajampeleka mahabusu ya magereza hapo ndio kuna kizunguzungu tunaendelea kufuatilia hili limetokea Mwandambo lisije kutokea tena la kituo cha polisi kugeuzwa mahabausu ya magereza.”

About The Author

error: Content is protected !!