
Rais wa Marekani, Donald Trump
SHIRIKA la Kimataifa la Kutetea Haki za Binaadamu la Amnesty International limetoa ripoti yake ya kila mwaka na kukosoa vikali hatua za rais wa Marekani, Donald Trump ambaye ametimiza siku 100 akiwa madarakani. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Amnesty imesema hatua za Trump zinalenga kurejesha nyuma mafanikio yaliyopatikana katika vita dhidi ya umaskini duniani, kupambana na ubaguzi wa rangi na vipaumbele muhimu vya haki za binadamu.
Tangu alipoapishwa kuongoza muhula wa pili tarehe 20 Januari 2025, Trump amechukua hatua kadhaa ambazo zimeutikisa ulimwengu kiuchumi, kijamii na kiusalama.
Baadhi, ni hatua za ushuru, kusitisha misaada ya kimataifa, sintofahamu na washirika wake wa NATO pamoja na vitisho vya kunyakuwa maeneo kama Gaza, Greenland, Mfereji wa Panama na kutaka kuifanya Canada kuwa jimbo la 51 la Marekani.
ZINAZOFANANA
Kardinali Becciu ajiondoa kumchagua Papa mpya
Mume wa Marehemu mwimbaji wa Injili ahukumiwa kunyongwa
Matumizi ya kijeshi yaongezeka duniani kwa kiwango kikubwa