January 10, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Dk Slaa akamatwa usiku ‘mnene’ Dar

 

JESHI la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, linamshikilia kwa mahojiano aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Sweeden, Dk Willibrod Slaa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Slaa alikamatwa jana usiku nyumbani kwake Bweni na mpaka sasa Jeshi hilo halijaweka wazi tuhuma zinazomkabili mwanasiasa huyo ambaye pia amepata kuhudumu katika wadhifa wa Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mbunge wa Karatu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, mahojiano na mwanasiasa huyo yamekwenda vizuri na hivi sasa wanaangalia sheria zinasemaje ili wachukue hatua zaidi.

Hata hivyo kamanda Muliro hakuwa tayari kueleza kwa undani tuhuma zinazomkabili Dk Slaa ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali na viongozi wake.

About The Author

error: Content is protected !!