MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya uwepo kwa kimbuga ‘Chido’ kilichopo kaskazini mwa Madagasca na kwamba kimbunga hiko kina uwezekano wa kusogea kusini mwa Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa hiyo iliyotolewa na TMA jioni hii imesema kuwa Kimbunga hicho hakiiashirii athari za moja kwa moja nchini lakini imetoa tahadhari ya kuwepo kwa mvua kubwa itakayoambatana na upepo pamoja na mawimbi makubwa ya bahari hususan katika maeneo ya Mkoa wa Mtwara.
” Upo uwezekano wa mvua kubwa za vipindi vifupi, upepo mkali na mawimbi makubwa ya bahari katika maeneo ya Mtwara na jirani kati ya tarehe 14 na 16 Desemba 2024″
Mamlaka hiyo imetoa tahadhari kwa watumiaji wa bahari na watu maeneo hayo kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri wa hali ya hewa unatolewa na TMA pamoja na kusikiliza ushauri wa wataalamu wa kisekta .
TMA imesema kuwa itaendelea kufuatilia mwenendo wa Kimbunga hicho na kuendelea kutoa taarifa.
ZINAZOFANANA
Bilionea na kiongozi wa kiroho Aga Khan afariki dunia
Ndoa ya Ramovic na Yanga yavunjika baada ya siku 80
Kauli ya Rais Samia yawaliza watoto wa Jenerali Kiwelu