January 15, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

TMA yatoa tahadhari uwepo wa kimbunga Chido

 

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya uwepo kwa kimbuga ‘Chido’ kilichopo kaskazini mwa Madagasca na kwamba kimbunga hiko kina uwezekano wa kusogea kusini mwa Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo iliyotolewa na TMA jioni hii imesema kuwa Kimbunga hicho hakiiashirii athari za moja kwa moja nchini lakini imetoa tahadhari ya kuwepo kwa mvua kubwa itakayoambatana na upepo pamoja na mawimbi makubwa ya bahari hususan katika maeneo ya Mkoa wa Mtwara.

” Upo uwezekano wa mvua kubwa za vipindi vifupi, upepo mkali na mawimbi makubwa ya bahari katika maeneo ya Mtwara na jirani kati ya tarehe 14 na 16 Desemba 2024″

Mamlaka hiyo imetoa tahadhari kwa watumiaji wa bahari na watu maeneo hayo kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri wa hali ya hewa unatolewa na TMA pamoja na kusikiliza ushauri wa wataalamu wa kisekta .

TMA imesema kuwa itaendelea kufuatilia mwenendo wa Kimbunga hicho na kuendelea kutoa taarifa.

About The Author

error: Content is protected !!