RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua rasmi Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kati ya Mwezi Mei/Juni 2025 mara baada ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuijadili na kuidhinisha Rasimu ya Dira ya Maendeleo 2050. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amewaambia wanahabari kuwa maandalizi ya Dira 2050 yanaenda sambamba na maandalizi ya mpango Elekezi wa muda mrefu wa maendeleo utakaotafsiri maono na matamanio yaliyopo kwenye Dira 2050, akiwataka wananchi kushiriki kikamilifu kwenye uzinduzi huo.
Akizungumzia tathimini ya Mchakato wa uandaaji wa Dira 2050, Waziri Kitila amesema matamanio na matarajio ya Watanzania wengi kwa miaka 25 ijayo ni kuona uchumi imara, unaostawi na unaoboresha Maisha yao huku pia wakitaka huduma bora, utoaji haki pamoja na uthabiti kwenye ulinzi na usalama.
Aidha wananchi wengi pia wametaka kuimarishwa kwa maendeleo ya Teknolojia na ubunifu, ulinzi na matumizi endelevu ya rasilimali za Taifa.
Aidha kulingana na Waziri Kitila Mkumbo, wananchi wengi pia wametaja sekta tano muhimu wanazotaka zitiliwe mkazo kwa miaka 25 ijayo ambazo ni pamoja na Kilimo, uzalishaji viwandani, miundombinu, huduma bora za kijamii, madini, mafuta pamoja na Gesi.
ZINAZOFANANA
Ushindi wa Profesa Lipumba wapingwa
Sativa amlipia Lissu fomu ya kugombea Uenyekiti Chadema
John Tendwa afariki dunia