Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Afrika kusini si salama tena kama zamani -Msangi

 

MWANAHARAKATI na kiongozi wa Watanzania wanaoishi Afrika Kusini, Mohammed Taliban Msangi, ametoa wito kwa vijana wa Tanzania kutafakari upya safari ya kwenda kutafuta maisha nchini humo, akieleza kuwa kwa sasa si mahali salama kama ilivyokuwa awali.Anaripoti Zakia Nanga,Dar es Salaam ….(endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Digital kuhusu hali inayoendelea Msangi amesema mazingira ya Afrika Kusini yamebadilika, hasa kutokana na vitendo vya ukatili vinavyowalenga wageni, jambo linaloweka maisha ya wengi hatarini.

“Kwa sasa siyo salama kama zamani, na hata utafutaji wake si ule wa awali,hata fursa zenyewe zimepungua, Vijana waache kufikiri kuwa Afrika Kusini bado ni sehemu ya matumaini makubwa kama ilivyokuwa zamani,” amesema Msangi

Kutokana na hali hiyo, amewashauri vijana kubadilisha mtazamo na kuanza kuangalia fursa zilizopo ndani ya Tanzania au katika nchi nyingine zenye mazingira bora na salama zaidi.

Aidha Msangi amesisitiza umuhimu wa vijana kuwa na mtazamo chanya kuhusu fursa zilizopo nyumbani, akieleza kuwa maendeleo yanaweza kupatikana popote pale iwapo kutakuwa na juhudi, ubunifu na mshikamano.

Kwa undani wa taarifa hii tembelea katika ukurasa wetu wa youtube ya @MwanaHALISI TV

About The Author

error: Content is protected !!