Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

LHRC yafuatilia kukamatwa kwa mwandishi wa habari Aloyce Nyanda

 

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimepokea taarifa za kukamatwa kwa mwandishi wa habari, Aloyce Nyanda, na Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Nyanda anadaiwa kukamatwa tangu 22 Aprili 2026, kwa tuhuma ambazo hadi sasa hazijawekwa wazi na mamlaka husika.

LHRC imesema inaendelea kufuatilia kwa karibu suala hilo, ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua stahiki za kisheria ili kuhakikisha haki inazingatiwa.

Aidha, taasisi hiyo imelitaka Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza kuhakikisha kuwa Nyanda anapatiwa haki ya dhamana kwa mujibu wa sheria, au afikishwe mahakamani haraka iwezekanavyo ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

About The Author

error: Content is protected !!