MSAJILI wa Vyama vya Siasa, Jaji (Mstaafu) Francis Mutungi, leo jijini Dar es Salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Umoja wa Afrika (UNOAU), Parfait Onanga-Anyanga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Katika mazungumzo hayo, Jaji Mutungi alimweleza mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Amesema hatua hizo zililenga kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa na mazingira bora ya demokrasia ya vyama vingi pamoja na kuimarisha ushirikiano na vyama vya siasa nchini.
Mazungumzo hayo pia yalijikita katika kuangalia namna taasisi mbalimbali zinavyoweza kushirikiana katika kuimarisha misingi ya utawala bora, demokrasia na amani nchini na barani Afrika kwa ujumla.
ZINAZOFANANA
Hatutaongeza bei ya gesi – Taifa Gas
Prof. Kabudi amrihi Lukuvi, Mgombea Mwenza wa NCCR- Mageuzi, azawadiwa ubunge
Mafuta yakipanda, mzigo unaangukia walala hoi, hii itaisha lini?