SHAHIDI wa 14 alitambulishwa mahakamani kama ‘P9’ (38), ameieleza Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam kuwa tarehe 22 Aprili aliitwa polisi na kutakiwa ahojiwe kama shahidi. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Shahidi huyo aliyetoa ushahidi wake kwenye kesi Na. 19605/2025 ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Ameyaeleza hayo leo tarehe 19 Februari 2025 alipokuwa anatoa ushahidi wake mbele ya jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Dustan Ndunguru akishirikiana na Jaji James Karayamaha na Jaji Ferdinand Kiwonde.
Mkazi wa Mbeya shughuli zake ni fundi umeme.
Amedai kuwa alianza kuvutiwa na siasa 2024 na chama alichovutiwa nacho ni Chadema kutokana na sera zake na kwamba alivutiwa kuwa mfuasi wa Chama hicho.
Shahidi huyo anadai kuwa alianza kufuatilia kwa karibu, mikutano na hotuba za viongozi wa Chadema.
P9′ ameieleza mahakama kuwa ameshiriki maandamano ya amani yaliyofanyika Mbeya yakiongozwa na viongozi watatu wa Chadema.
Anadai kuwa kundi moja Uyole mpaka Kabwe liliongozwa na Lissu wengine Isanga mpaka Kabwe liliongozwa na John Heche na wengine njia ya Airport Songwe yakielekea Kabwe akadai amesahau.
Amedai kuwa tarehe 3 Aprili 2025 usiku akiwa nyumbani kwake alikuwa aliperuzi kwenye mtandao kwa kutumia simu yake, aina Samsung 8 Pro kwenye ukusara wa Instagram.
Akiuelezea mtandao wa Instagram amedai kuwa ni mtandao ambao ili uiingie lazima uwe na simu janja ‘smartphone’, pia uwe na akaunti .
Anadai kuwa mtandao huo watu wanaweka picha na video, na kwamba wakati anafungua aliona Video ya Lissu kupitia mtandao huo.
Anadai kuwa aliona Video ambayo Lissu akihamasisha vurugu za kuzuia uchaguzi mkuu akiwa ukumbini, akiwa amevalia Kombati ya Kaki ya Chadema.
Shahidi huyo alidai kuwa amemsikia Lissu akidai kuwa atauvuruga uchaguzi huo na kuzuia kwa kufanya vurugu, ‘atakichafua’.
Anadai kuwa alihamasika “Niliona kuwa ipo haja ya kufanya hivyo”
P8 ameendelea kudai kuwa tarehe 4 Aprili 2025 akiwa nyumbani kwake walikuwa wanajadili hotoba ya Lissu yeye na jirani zake “tukawa tunajadili kama Mheshimiwa amesema tukichafue tukawa tunajadili tunafanyaje”.
Anadai kuwa kuna mtu ambaye anakutana naye ambaye hamjui jina alimuomba namba yake ya simu.
Anaendelea “tarehe 5 Aprili majira ya asubuhi nikiwa nyumbani nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kama mteja anayehitaji fundi umeme na kufanyika shughuli za umeme nyumbani kwakeni”
Shahidi anaeleza kuwa mteja huyo aliomba kuonana naye, “Nilikwenda sehemu tuliyokubaliana nikaenda nilivyofika akajitambulisha kuwa yeye ni ofisa wa polisi na akanionesha kitambulisho chake cha kazi akisema anatokea kituo cha polisi cha mwanjera akaniweka chini ya ulinzi na kuniambia kuwa tutaongoza mpaka kituo cha polisi na kwamba natuhumiwa kufanya uchochezi kutaka kuzuia uchaguzi.”
Ameieleza mahakama kuwa alipofikishwa kituo cha polisi alihojiwa na baadaye majira ya mchana wakaja ndugu zake kumdhamini na kutolewa.
Anadai kuwa tarehe 22 Aprili alipigiwa tena simu na mtu aliyejitambulisha kuwa yeye ni polisi na kwamba anahitajika kituoni “Nikaenda kituoni wakaniambia kuwa wanataka kunihoji kama shahidi”
Shahidi huyo ameieleza kuwa alihojiwa kuhusu suala kuzuia uchaguzi kwamba lilianzaje na ilikuaje na kwanini walikata na wenzake kujadili “walinihoji kuhamasisha kuzuia uchaguzi.”
Anadai kuwa alieleza alipokuwa alihojiwa kuwa aliona clip (video fupi) aliyomuonesha Lissu akizungumza.
Kesho saa tatu asubuhi ambapo Lissu atamuuliza maswali ya dodoso (cross examination).
ZINAZOFANANA
Mahkama Z’bar yatupa kesi za uchaguzi
Kesi ya Lissu: Shahidi aeleza alivyomkamata aliyehamasisha vurugu za uchaguzi
EACOP yakabidhi karakana na vifaa vya mafunzo katika chuo cha Don Bosco