February 17, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Tundu Lissu atumia PGO kumbana shahidi wa tisa

Tundu Lissu akiwa mahakamani

 

TUNDU Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ametumia kitabu cha muungozo wa Jeshi la Polisi ‘PGO’ kumbana kwa maswali shahidi wa tisa kwenye kesi ya uhaini Na. 19605/2025 inayomkabili mahakamani hapo. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Mbele ya jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru anayeshirikiana na Jaji James Karayamaha n Ferdinand Kiwonde. Shahidi wa tisa Ofisa wa jeshi la polisi ASP Geofrey Lutufye (47) aliyeoongozwa na Wakili wa serikali Mwandamizi Renatus Mkude.

ASP Lutufye ameieleza mahakama kuwa kazi yake ni upelelezi anafanya kazi ofisi ya mkuu wa upelelezi mkoa wa Arusha akiwa kiongozi wa kikosi cha Anti Robbery “kikosi cha kuzuia uhalifu kama vile uporaji”.

ASP Geofrey Lutufye ameieleza mahakamani hapo kuwa tarehe 28 Aprili 2003 alipata mafunzo ya katika chuo cha polisi Moshi. “Nilijifunza upelelezi na mafunzo mengine mbalimbali, nilimaliza mwezi wa 11, 2003.”

“Mafunzo mengine nilipata ya nyota ya kwanza, nilisomea chuo cha polisi Moshi ilikuwa ni mwaka 2013 na baadae mafunzo ya cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Polisi nililipata chuo Dar es salaam polisi Academy hapa Dar es salaam nilimaliza mwezi wa 11 mwaka 2023,” alidai.

Aliieleza mahakama kuwa alipata mafunzo mbalimbali ya akiwa kazi na kwamba anauzoefu wa miaka 15 katika majukumu yake ya upelelezi.

ASP Lutufye alidao kuwa alianzia kazi kwenye kituo cha Polisi cha Oysterbay Dar es Salaam, nilianza kama general duty na baadae nikapelekwa Geita ofisi ya upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Geita ndiyo nikahamia Mkoa wa Arusha.

ASP Lutufye ameieleza mahakama hiyo kuwa jukumu lake ni kufanya doria mbalimbali, kukamata watuhumiwa, kufanya upelelezi na kuwafikishia mahakamani.

ASP Lutufye anaeleza kuwa tarehe 3 Aprili 2025 akiwa kwenye doria na kikosi chake chenye askari 9 walipokea maelekezo kuwa kuna watu wanapanga uhalifu “tulikuwa tunafanya doria tukiwa tunatumia gari la polisi aina ya Toyota Landcruiser na nikapata maelekezo kutoka kwa kaimu mkuu wa upelelekezi ASP Bonny Mgogo”

ASP Lutufye anadai kuwa maelekezo hayo yaliwataka waende kijiwe cha bajaji kilichopo kwa Mrombo ambapo kuna vijana wanahamasishana kuzuia uchaguzi wa mwaka 2025.

“Nilikuta vijana wakila njama za kuzuia uchaguzi mkuu 2025”

ASP Lutufye anadai kuwa waliwakamata vijana wawili ambapo ni P4 na P7 “Nilitoa maekekezo wapelekwe kituo cha Polisi Murieti, hao askari ni wanne, kituo cha Murieti kipo mkoa wa Arusha.

Anadai kuwa alipewa maelekezo wawapeleke P4 na P7 kwenye ofisi ya mkuu wa upelelezi.

“Tukiwa njiani tunawapeleka P4 na P7 niliwahoji kwamba kwanini mnahusika kula njama kutaka uchaguzi mkuu wa 2025 usifanyike?

“Wote walikiri kuwa wanamuunga mkono Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu kutokana na ile kauli yake aliyoitoa kwenye mtandao kuwa atazuia uchaguzi, ataleta uchochezi na atakinukisha.”

Anaeleza kuwa alipewa tena maelekezo afungue jalada la Uchunguzi, “nilifungua jalada hilo ambalo ni ARS/D/CID/B/40/2025”. Anadai kuwa alipewa maelekezo mengine ya kuwahoji watuhumiwa hao naye akayashusha maelekezo hayo kwa askari wengine. Naye aliandika maelezo yake ya ushahidi tarehe 18 Aprili 2025.

Sasa ni zamu ya Lissu kumuuliza maswali ya dodoso kwa shahidi.

Lissu: Sasa waeleze majaji, huko polisi mnakojifunzia hizi kazi huwa mnafundishwa kuwa waongo?

ASP Lutufye: Hatufundishwi kuwa waongo.

Lissu: Waeleze majaji kama huwa mnafundishwa mnapotoa ushahidi mahakamani kuongeza maneno ambayo hayapo?

ASP Lutufye: Hatufundishwi.

Lissu: Waeleze majaji kama huko Polisi mnafundishwa kutokuwa na heshima?

ASP Lutufye: Sio kweli.

Lissu: Waeleze majaji kama huko polisi mnafundishwa kuwa watu wasio na maadili?

ASP Lutufye: Sio kweli

Lissu: Sio kweli nini sasa?

ASP Lutufye: Tunafundishwa kuwa watu wenye maadili.

Lissu: Unafahamu kitu kinaitwa PGO?

ASP Lutufye: PGO naifahamu.

Lissu: Waeleze majaji kama ni sahihi au sio sahihi kwamba PGO inasema askari wanapaswa kuwa weledi kwenye kazi zao?

ASP Lutufye: Ni kweli inasema hivyo.

Lissu: Sasa narudi kwenye PGO ulieleza mahakama kuwa uliandindika maelezo yake tarehe 18 Aprili 2025 ?

ASP Lutufye: Kweli.

Lissu: Na unaweza kuyatambua?

ASP Lutufye: Ni kweli.

ASP Lutufye anapewa maelezo yake na kuyakubali.

Lissu: Waeleze majaji ni nani aliyekuandikia hayo maelezo?

ASP Lutufye: Maelezo niliandika mwenyewe.

Lissu: Nani aliyekupa onyo wakati unaandika?

ASP Lutufye: Mimi shahidi

Lissu: Nauliza nani alikupa onyo.

ASP Lutufye: Niliandika mwenyewe.

Lissu: Nani alikushuhudia.

ASP Lutufye: Hakuna aliyenishuhudia.

Lissu: Naomba nimsomee maelezo yake ili nionesha huyu shahidi ni muongo hafai kuamimiwa.

Lissu: Nakusomea maelezo yako kama kuna sehemu nimekosea.

Lissu: Anayasoma

Lissu anamueleza kuwa maeneo 13 ya maelezo yake aliyoyaandika polisi kama shahidi na yale aliyoyaeleza mahakamani.

Kabla ya kuendelea na hatua hiyo Lissu amemuuliza shahidi huyo kama angependa maelezo yake yawe sehemu ya kielelezo cha kesi hiyo naye akakibuli maelezo yake yapokelewe hatua hiyo imemfanya Lissu kuwa na vielelezo vinane alivyotanguliza mahakamani hapo na kielelezo hicho kipewa alama ‘D8’.

Inaendelea

About The Author

error: Content is protected !!