Tundu Lissu akiwa mahakamani
MWENYEKITI wa chama kikuu cha upinzani nchini, Tundu Lissu, amerejea tena mahakamani leo Jumatatu, baada ya kuahirishwa Ijumaa iliyopita. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mamia ya wafuasi wa chama chake – CHADEMA, wamejitokeza kusikiliza kesi yake ya uhaini inayomkabili mwenyekiti wao.
Shahidi atakayesikilizwa leo ni shahidi P2 ambaye ni shahidi wa kificho na ataanza kwa kujitambulisha kuwa ana miaka 38 na dini yake ni mkristo.
Shahidi huyo alianza kuhojiwa na upande wa mashtaka na kuanza kujitambulisha kuwa anatokea Songea, mkoani Ruvuma na ni mfuasi wa Chadema tokea mwaka 2021.
Anasema huwa anashiriki kwenye mikutano mbalimbali ya chama akiwa kama mwanachama wa chama hicho.
Anasema, tarehe 4 Aprili 2025, alikuwa kwenye manispaa ya Songea akifanya shughuli zake za kawaida na wakati anapitia mitandao ya kijamii alikutana na video za kisiasa kuhusiana na mkutano wa Lissu jijini Dar es salaam.
Shahidi: Katika maelekezo hayo alisisitiza uchaguzi usifanyike kama njia ya kuleta mageuzi. Baada ya video hiyo nilipata kujua namna jambo hilo litatekelezwa na nikanza kutafuta viongozi ili kupata uelewa zaidi.
Upande wa mashtaka: Nini kikaendelea?
Shahidi: Nikamtafuta mwenyekiti wa vijana wa CHADEMA, wilayani Songea, Esau Chiza, kujua nini kitaendelea.
Upande wa mashitaka: Baada ya kumtafuta nini kiliendelea?
Shahidi: Tarehe 7 Aprili 2025 ,nilitoa mchango wa shilingi 10,000 kwa ajili ya ziara ya mheshimiwa Lissu kwenye mkoa wetu wa Ruvuma.
Upande wa mashataka: Nini kiliaendelea?
Shahidi: Tarehe 9 Aprili nikiwa kwenye shughuli zangu ndiyo nikaona kwenye taarifa ya habari Mheshimiwa Lissu alikamatwa, lakini ilipofika tarehe 10, nilijianda kwenda kwenye mkutano ilikupata ufafanuzi nilipofika nilikutana na magari ya polisi.
Upande wa mashitaka: Baada ya kuona hivyo ukafanya nini?
Shahidi: Nilifika kwenye ofisi za CHADEMA mjini Songea nikawasiliana na wanachama wengine nikaambiwa makamu mwenyekiti atazungumza na wanachama kutoa ufafanuzi kwa nini mkutano haukufanyika na kwa nini mwenyekiti alikamatwa.
Upande wa mashitaka: Huyo Makamu mwenyekiti ni nani?
Shahidi: Makamu Mwenyekiti ni John Heche.
Baada ya maelezo ya upande wa mashitaka na shahidi kumaliza kutoa Ushahidi wake, Jaji ameruhusu Lissu kuanza kumuuliza maswali shahidi.
Lissu: Shahidi unanisikia sawa sawa?
Shahidi: Hapana sikusikii
Lissu: Na kelele zote hizi unisikii?
Shahidi: Nakusikia
Lissu: Swali langu la kwanza waelezee majaji kama uliandika maelezo polisi
Shahidi: Nilichukuliwa maelezo polisi
Lissu: Ndiyo haya maeleo ya tarehe 22 Aprili 2025, uliyasaini maelezo hayo.
Shahidi: Ndiyo nilisaini.
Lissu: Je ukioneshwa maelezo hayo utayatambua?
Shahidi: Ndiyo.
Lissu: Naomba shahidi aonyeshwe maelezo ya tarehe 22 Aprili 2025.
Lissu: Naomba nikusome maelezo uliyoyasaini polisi baada ya hapo nitauliza maswali
Dakika 18 zilizopita”…umesema watazuia uchaguzi je, unajua ni namna gani watazuia uchaguzi?”, Wakili auliza
Upande wa mashataka: Nini kiliendelea huko mjini?
Shahidi: Nilipofika pale niliona viongozi wa kitaifa wa chama wakiita waandishi wazungumze nao lakini wakaingia polisi na kutuweka chini ya ulinzi. Katika purukushani nikajikuta nimekamatwa na kupelekwa kituo cha polisi karibu na ofisi ya mkuu wa mkoa Ruvuma.
Upande wa Mashataka: Nini kiliendelea kituoni?
Shahidi: Niliwekwa maabusu na baadaye nikahojiwa na polisi juu ya tuhuma nilizokutwa nazo
Wakili: Nini kiliendelea?
Shahidi: Baada ya kuchukuliwa maelezo niliachiliwa kwa dhamana nikaambiwa niripoti kila jumatatu kituoni.
Wakili: Nini kiliendelea?
Shahidi: Nilianza kuripoti pale polisi lakini siku ya Jumatatu iliyofuata nilipangiwa kuja siku nyingine maana ilikiwa siku ya Pasaka.
Wakili: Umekuwa ukimtaja Tundu Lissu kama mwenyekiti wa chama, Je, unamfahamu vipi ukiwa Songea?
Shahidi: Ni mwanasiasa na nimekuwa nikimfahamu kwenye mitandao ya kijamii na harakati za chama pale alipotangaza kugombea uwenyekiti ndipo nilipoanza kuwa mfuasi wake.
Wakili: Katika maelezo yako umesema watazuia uchaguzi je unajua kwa namna gani watazuia uchaguzi?
Shahidi: Nilikiwa sijui.
ZINAZOFANANA
Lissu alivyombana shahidi wa sita, awasubiri wengine kesho
RITA yatoa mafunzo ya usimamizi wa mirathi, utatuzi wa migogoro kwa Viongozi wa Serikali, wazee wa kimila
Lissu avuna kielelezo kingine kutoka serikalini