Tundu Lissu akiwa mahakamani
MAHAKAMA Kuu, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, kesho tarehe 16 Februari 2026 itaendelea na usikilizaji wa kesi Na.19605/2025. Upande wa Jamhuri unatarajia kuendelea kuwasilisha mashahidi wake ambapo kesho wataaendelea na ushahidi wa shahidi wa saba. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Tayari mashahidi sita washatoa ushahidi wao katika Mahakama hiyo mbele ya jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru akishirikiana na Jaji James Karayamaha na Jaji Ferdinand Kiwonde .
Mashahidi wa serikali waliotoa ushahidi wao ni pamoja na George Bagyem Naibu Mpelelezi wa Kanda ya Dar es Salaam (DZCO), John Kaaya Mpelelezi dawati doria ya mtandaoni ,Samweli Kaaya Mtaalamu wa Sayansi ya uchaguzi wa picha na video wa jeshi la Polisi na .
Shahidi wa nne ni shahidi wa siri aliyepewa utambulisho wa P5 na shahidi wa tano P6 huku shahidi wa sita akiwa ni ofisa wa Polisi Koplo Michael.
Wiki iliyopita ijumaa shahidi wa serikali Koplo Michael alitao ushahidi wake akiongozwa na Wakili wa Serikali Ignas Mwinuka.
Koplo Michael alieleza mahakamani hapo kuwa aliaanza kazi upelelezi mkoani Kilimanjaro tangu mwaka 2015.
“Nimejiunga Jeshi la Polisi mwaka 2012 na kuhitimu mwaka 2013, nilipata mafunzo ya awali katika shule ya Polisi Tanzania TPS kwa maana ya Shule ya Polisi iliyopo Moshi,”alidai.
Amedai kuwa Tarehe 8 Aprili 2025, yeye na askari wenzake walipata taarifa za kiintelejensia katika eneo la Njoro, Moshi mjini .
“Tukiwa tumefika maeneo ya Njoro hapo wilayani Moshi, tulipata taarifa za kiintelijensia kuwa kuna kijana mmoja anahamasisha wenzake kuhusiana na kufanyika na Uchaguzi Mkuu uliokuwa unatarajiwa kufanyika mwaka 2025,”.
Amedai kuwa walipomhoji kijana huyo alisema yeye ni mkereketwa wa Chadema na alikuwa anaunga mkono kauli ya Mwenyekiti wake wa Chama Tundu Lissu ndio maana alikuwa anahamasisha fujo na kukinukisha.
Alidai kuwa kijana huyo alidhamiria kufanya uasi kwa serikali inayoongozwa na CCM na aliongeza kwa kusema kuwa Mwenyekiti wao alisema hawatakubali uchaguzi kufanyika.
Na wako tayari kukinukisha hadi Serikali watakapofanya marekebisho ya tume huru ya Uchaguzi pamoja na Katiba Mpya.
Baada ya kumuandika maelezo nilimpa ayasaini kila page na akakubali kuwa ni malezo yake.
Lissu akaanza kumuuliza maswali ya dodoso shahidi huyo kama ifuavyo:-
Lissu: Sasa Koplo Michael unakumbuka ulitoa maelezo yako na unaweza kuyatambua ukiyaona?
Koplo Michael : Ndio naweza.
Koplo Michael: Haya maelezo ni ya tarehe 22/04 nimeyatambua yana sahihi yangu.
Lissu ameyasoma maelezo ya shahidi na kumuuliza kama maelezo hayo ni yake naye akakiri kuwa ni yake.
Lissu: Je uko tayari yapokelewe kuwa ushahidi Mahakamani?
Koplo Michael: Maelezo haya niliandika kwa kifupi tu.
Lissu: Wewe Polisi jibu swali langu usilete stori za line polisi hapa. Uko tayari yapokelewe? Jibu ndio au hapana?
Koplo Michael: Kama Jamhuri wataridhia sina pingamizi.
Jaji Ndunguru: Yatakuwa ni ‘D5’ Yaani ushahidi wa utetezi namba 5.
Lissu: Naomba apewe D5.
Anapatiwa hapa.
Lissu: Kwamba ni askari Polisi toka mwaka 2015 yapo kwenye maelezo yako?
Koplo Michael: huo mwaka hakuna kwenye maelezo yangu.
Lissu: Ulijiunga 2012 na 2013 ukafuzu jeshi la polisi
Koplo Michael: Sikuyaandika hayo.
Lissu: Sema kwa sauti we polisi.
Koplo Michael: Nimesema kwa sauti mbona.
Lissu: Kuhusu shule ya polisi Tanzania iliyopo Moshi
Koplo Michael: Hayo hayapo kwenye maelezo yangu.
Lissu: Hivi kwanini hujibu ki askari? Nataka ujibu kama askari.
Koplo Michael: Anachekacheka kama anataka kulia.
Lissu: Tarehe 08 Aprili 2025, ulimpeleka ofisi ya RCO na kukuelekeza ufungue faili la uchunguzi. Ulisema ahojiwe na awekwe mahabusu hadi mtakapopata maelekezo mengine. Yapo kwenye maelezo?
Koplo Michael: Maneno kuwa awekwe mahabusu hadi yatakapotolewa maelekezo mengine sikuliandika.
Lissu: Ulisema sharti la mtuhumiwa kuripoti kila jumatatu. Yapo hayo kwenye maelezo yako?
Koplo Michael: Hakuna.
Lissu: Kuhusu kumtafuta P8 na kumuhoji maelezo kama shahidi.
Koplo Michael: Kuna mambo hayapo hapo.
Lissu: Hivi ulisema alikuwa anaripoti jumatatu?
Koplo Michael: ndio.
Lissu: Tarehe 22 ilikuwa jumangapi?
Koplo Michael: Ilikuwa jumanne lakini alikuja kuripoti jumanne kwasbaabu
Lissu: Hiyo kwasababu mpelekeee RCO wako kule Kilimanjaro mimi jibu langu limetosha kuwa ilikuwa jumanne.
Lissu: Maelezo ya kuunga mkono kauli ya Chama uliandika?
Koplo Michael: Sikuandika lakini
Lissu: Nimekwambia lakini zako utawaeleza waandishi wa habari baadae au mapolisi wenzako sio hapa.
Lissu: Wewe askari mimi nimefundishwa kukamata waongo.
Koplo Michael : Mimi pia ni mtaalamu mheshimiwa.
Lissu: Wewe sio mtaalamu wa chochote ndio maana ni Koplo wa polisi. Ungekuwa mtaalamu usingekuwa Koplo.
Lissu: Hivi umeeleza sababu ya maelezo yako polisi na uliyosema mahakamani.
Koplo Michael: Sijaeleza sababu kwasababu hakuna utofauti.
Lissu: Unasema ulimkamata P8 na kumpeleka kituoni. Halafu RCO akakwambia ufungue shauri.
Koplo Michael: Hata sikuelewi yani.
Lissu: kwahiyo ulimkamata ukiwa tayari una faili la uchunguzi?
Koplo Michael: Sio kweli nilifungua baada ya kuwa nimeshamkamata.
Lissu: Kupanga kufanya vurugu ni kosa?
Koplo Michael: Sahihi.
Lissu: Kwahiyi P8 alikuwa amefanya kosa?
Koplo Michael: ni kweli alikuwa amefanya makosa
Lissu: Kwa hiyo maelezo yake hayapo?
Koplo Michael: Sijayaleta
Lissu: Je mlifungua kesi?
Koplo Michael: Hatukufungua kesi.
Lissu: Hadi leo hamjafungua?
Koplo Michael: Sijui kwakweli.
Lissu: RCO ndio alikwambia chukua maelezo ya shahidi kwenye kesi ya Lissu.
Koplo Michael: Hapana sio hivyo.
Lissu: Anamsomea alipoandika kuwa shahidi kwenye kesi ya lissu.
Koplo Michael: Ni kweli nilisema kumbe.
Lissu: Kwahiyo mlikuwa mnaandaa kesi ya Lissu?
Koplo Michael: Sio kweli.
Lissu: Kwahiyo mlikuwa mnaandaa nini?
Koplo Michael: Ushahidi wa kesi.
Lissu: Kesi gani?
Koplo Michael: hii ya kwako.
Lissu: Kumbe ni yangu umebana umeachia.
Lissu: Nilitishia serikali kwasababu nilisema tutazuia uchaguzi, wambie majaji ni wapi umesema neno lolote juu ya maneno niliyosema?
Koplo Michael : Mimi nilisema aliyoniambia shahidi.
Lissu: Umeelewa swali we polisi?
Koplo Michael: Hapana sijasema lolote kuhusu maneno gani ulisema.
Lissu: Maambiwa nilichapisha maneno mitandaoni sasa sema kama kwenye kielelezo D5 kama ulisema chochote kuhusu maneno yangu niliyochapisha.
Koplo Michael: Hapana sikuandika lolote kwenye hayo.
Lissu: Kutaka mabadiliko ya Katiba, Yume Huru ya Uchaguzi ni kosa la jinai?
Koplo Michael: Sio kosa la jinai.
Lissu: Kuhamasisha wananchi nchi nzima kupatikana Katiba Mpya na kuzuia uchaguzi ni kosa?
Koplo Michael: ni kosa
Mhe. Lissu: Kosa gani?
Koplo Michael: Mimi sio mtaalamu wa sheria, wanasheria watasema.
Lissu: Huna unalojua wewe ni Koplo tu, umetaja Katiba tutajie ibara sasa?
Koplo Michael: Sijui kosa ambalo umeshitakiwa nalo.
Lissu: Waheshimiwa sina swali lingine kwa shahidi huyu.
Jaji Ndunguru: Re Examination (maswali ya kusawazisha).
Wakili Ignas anaendelea…
Wakili Iganas: Je uliposema hakuna utofauti ulimaanisha nini?
Koplo Michael: Nilimaanisha hakuna tu tofauti maana ni ile ile.
Wakili Ignas: Je ulisema hujui anashitakiwa na kosa gani? Ulimaanisha nini?
Koplo Michael: Najua ni uhaini lakini uhaini ni mpana unajumuisha uchochezi na kuharibu mali.
Wakili Iganas: ni hayo tu Mheshimiwa.
Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka mnasemaje?
Renatus Mkude: Tunaomba tuendelee Jumatatu.
Jaji Ndunguru: Kwanini msiendelee na shahidi mwingine atakapoishia ikifika saa 11 tunaacha.
Mkude: Mheshimiwa Jaji naomba tuendelee jumatatu tafadhali muda umeenda.
Jaji Ndunguru: Basi jumatatu saa tatu kamili asubuhi tukutane.
Shauri litaendelea kesho saa tatu asubuhi.
ZINAZOFANANA
Siku ya Kimataifa ya Wanawake 2026 yasherekewa kwa Kishindo- Kilombero Sugar
Dk. Nchimbi ataka wizara zishirikiane kuimarisha uhifadhi wa mazingira
Jaji Mutungi akutana na Mwakilishi wa UN