WAZIRI wa Mambo ya Ndani wa Benin, Alassane Seidou, ametangaza kuwa jaribio la mapinduzi lililofanywa na “kikundi kidogo cha wanajeshi” limezimwa na jeshi la nchi hiyo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea). Akizungumza kupitia televisheni ya taifa, Seidou aliwahakikishia wananchi kuwa hali imedhibitiwa na hakuna tishio la kuendelea kwa machafuko. Amewataka raia kubaki watulivu na kurejea katika shughuli zao za kila siku kama kawaida. Katika ujumbe wake, Waziri Seidou alisisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kufuatilia hali kwa karibu ili kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kutawala nchini Benin. Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Erasto Masalu See author's posts Post navigation Serikali ya Benin imepinduliwa Desemba 9, kutoka kushuhudia gwaride hadi kubaki nyumbani