AIRTEL Tanzania imemtangaza Jogrey Pascal Paul, mwalimu wa Jiografia kutoka Shule ya Sekondari Hai, kuwa mshindi wa tatu wa gari aina ya Mazda CX-5 kupitia kampeni yake ya “Mwaka Umenyooka na My Airtel Money App,” inayoendelea kuhamasisha matumizi ya huduma za malipo ya kidijitali nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mshindi huyo alichaguliwa katika droo iliyofanyika Aprili 14, 2026, na atakabidhiwa gari hilo baada ya kukamilika kwa taratibu za uhakiki.

Kampeni hiyo inalenga kuongeza matumizi ya My Airtel Money App kwa kuwahamasisha wateja kufanya miamala ya kila siku kama kutuma na kupokea pesa, kulipia bili, kununua muda wa maongezi na tokeni za umeme. Kila muamala unaofanyika kupitia app hiyo humuingiza mteja kwenye droo ya zawadi.

Paul anakuwa mshindi wa tatu wa Mazda CX-5 katika kampeni hiyo. Mshindi wa kwanza alikuwa Shakuu Joshua, dereva wa taxi kutoka Kimara-Temboni Dar es Salaam, huku mshindi wa pili akiwa Mohammad Raza Roshanali kutoka Arusha.

Mbali na magari, Airtel Tanzania ilisema pia imetoa washindi saba wa televisheni (TV sets), pamoja na mshindi mmoja wa pikipiki aina ya boda boda katika droo ya hivi karibuni.

Aidha, kampuni hiyo ilieleza kuwa wateja wengine saba wameshinda pikipiki kupitia sehemu nyingine za kampeni hiyo, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha matumizi ya huduma za fedha mtandao.

Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Lugamba, alisema kampeni hiyo inaendelea kuongeza matumizi ya malipo ya kidijitali huku ikiwatuza wateja waaminifu.

“Wateja wanazidi kutumia huduma za fedha mtandao kwa shughuli za kila siku, na kampeni hii imeongeza ushiriki kwa kiwango kikubwa,” alisema.

Airtel Tanzania imesema itaendelea kuboresha huduma zake za malipo ya kidijitali ili ziwe rahisi, salama na zinazopatikana kwa watu wengi zaidi nchini.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!