FILE - Benin's President Patrice Talon attends a meeting with Brazilian President Luiz Inacio Lula da Silva at Planalto presidential palace in Brasilia, Brazil, on May 23, 2024. (AP Photo/Eraldo Peres, File)
WAZIRI wa Mambo ya Ndani wa Benin, Alassane Seidou, ametangaza kuwa jaribio la mapinduzi lililofanywa na “kikundi kidogo cha wanajeshi” limezimwa na jeshi la nchi hiyo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Akizungumza kupitia televisheni ya taifa, Seidou aliwahakikishia wananchi kuwa hali imedhibitiwa na hakuna tishio la kuendelea kwa machafuko. Amewataka raia kubaki watulivu na kurejea katika shughuli zao za kila siku kama kawaida.
Katika ujumbe wake, Waziri Seidou alisisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kufuatilia hali kwa karibu ili kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kutawala nchini Benin.
ZINAZOFANANA
Serikali ya Benin imepinduliwa
Tanzania yaibuka kinara wa utalii duniani
TRA yawataka wanachama wa SACCOS kuhamasisha ulipaji kodi