CHAMA cha Wananchi (CUF), kimeanza maombolezo ya kitaifa ya siku 30 kwa ajili ya watu waliouawa, kujeruhiwa na kupotea tarehe 29 Oktoba 2025,siku uliofanyika uchaguzi mkuu. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza na Waandishi wa habari Mwenyekiti wa CUF, Prof.Ibrahimu Lipumba amesema bendera zote za chama hicho, zitapepea nusu mlingoti kwa kipindi hicho na watafanya ibada maalumu tarehe 10 Novemba 2025 kwa kufunga kula mchana na kufanya maombi .
Aidha Lipumba amesema watu wakiandamana hukumu yao sio kupigwa risasi bali ni kukamatwa na kupelekwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili kwa mujibu wa sheria.
ZINAZOFANANA
Mwanajeshi wa Marekani akamatwa na mabomu Tanzania
Machafuko ya 29 Oktoba: Maaskofu Katoliki wataka wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wawajibike
Shinikizo la kufanyika uchunguzi wa mauaji ya 29 Oktoba lashika kasi