October 24, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mahakama yakataa dhamana ya Lissu, Mwenyewe adai hakuna kesi

 

MAHAKAMA Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam, imelikataa ombi la Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, kutaka apewe dhamana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Lissu aliwasilisha hoja hiyo leo tarehe 24 Oktoba 2025, baada ya Jamhuri kuomba kesi iahirishwe kutokana na kutokuwa na shahidi kwa siku ya leo.

Lissu ameomba dhamana hiyo huku akinukuu kifungu cha kifungu 302(3) cha mwendendo wa makosa ya jinai.

Lissu ameieleza mahakama hiyo kuwa akipewa dhamana hiyo hatakwenda popote na kwamba atakuwepo kwa tu mtaani.

Lissu aidai kuwa uamuzi wa jana na juzi umeashiria kuwa hamna kesi dhidi yake na kwamba apewe dhamana hiyo ili asiendelee kuteseka gerezani.

Mwanasiasa huyo amedai kuwa sasa yupo gerezani kwa muda wa siku 202 yaani miezi sita na nusu na kwamba shtaka hilo analichukualia kuwa ni hatua ya uoga wa serikali .

Ameiambia mahakama kuwa kesi hiyo ipo ili uchaguzi mkuu upite jambo ambalo lilipingwa vikali na wakili wa serikali Renatus Mkude.

Mapema Jamhuri katika kesi hiyo ya uhaini inayomkabili Lissu, iliomba iahirishwe mpaka tarehe 3 Novemba 2025, kwa kuwa leo hawana shahidi.

About The Author

error: Content is protected !!